Taarifa iliyotolewa na wizara ya ulinzi wa Algeria imesema vikosi vya kupambana na ugaidi vya Algeria vimewaua waasi watano kwenye eneo la El Kseur mkoani Bejaia.
Habari zimesema bunduki tano aina ya Kalashnikov pamoja na magazini tatu zilikamatwa katika opresheni hiyo.
Mbali na hayo, Alhamisi ya wiki iliyopita vikosi vya jeshi vilianza opresheni kubwa katika misitu ya El Kseur, na kumuua gaidi mwingine.
Wapiganaji wachache wanaoshirikiana na tawi la Al-Qaeda katika eneo la Maghreb (AQIM) wameanzisha makundi yenye uhusiano na kundi la IS, na bado wamejificha kwenye maeneo ya jangwa karibu na Libya na Mali, na kuwa tishio kubwa la kigaidi kwa Algeria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni