chef Mishamo Tz
MAHITAJI
Tambi nyembamba mfuko 1 (200 g)
Samli vijiko 3 vya chakula
Maziwa mazito nusu kikopo (200g)
Zabibu kavu nusu kikombe
Arki ya vanilla kjk 1 cha chai
MATAYARISHO
1. Vunja vunja tambi ziwe ndogo ndogo sana
1. Teleka sufuria tia samli ikipata moto tia tambi
3.koroga uwe unazivunja vunja kwa mwiko mpaka ziwe brown kiasi (dakika 3-5) kwa moto wa kiasi
1. Tia maziwa mazito na zabibu kavu ,changanya
5.tia arki ,changanya kwa sekunde 30 au dkk 1 ,zima jiko
1. Tumia vikombe vya kahawa au kitu chochote kutolea shape, vipake mafuta, tia tambi zako zikiwa bado zamoto kikombe karibia kijae ,didimiza kwa kutumia kijiko weka pembeni
7.malizia zilobaki
8.baada ya dakika 1 au 2 vitoe taratibu, tumia ujiti kuanzia kutoa ukiona vinafanga tabu kutoka.
1. Vipange kwenye sahani
2. Enjoy.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni