Mishamo Tz

Ijumaa, 6 Oktoba 2017

Chapati za nazi


Chef Mishamo Tz

Mahitaji

unga wa ngano vikombe 4
tui la maji kikombe 1
yai 1 (si lazima )
chumvi kiasi
sukari kijiko 1 cha kula
mafuta ya kupikia vijiko 2 vya kula
maji robo kikombe

MATAYARISHO

1. changanya mahitaji yako yote isipokua maji, changanya kwa dakika 1 kwa kutumia mkono au machine

2. tia maji robo kikombe , kanda mpaka donge liwe laini, kadiri utakavokanda unga ukawa laini ndio kadiri chapati zitakavokua laini

3. donge lkiwa linanyata engeza unga wa ngano kiasi

4. utoe uweke sehem ya kukandia ugawe madonge madogo 5 sawa sawa na yafanye duara

5. chukua donge moja moja sukuma duara pakaza mafuta kijiko 1 juu ueneze, kunja kufanya mstari mwembamba na mrefu na ukunje duara

6. malizia zilobaki na ziwache zijivute kwa muda wa dakika 15 au Zaidi

7. weka chuma kwenye moto wa kiasi kikipata , sukuma chapatti moja moja na uchome upande 1 ukiwiva geuza wa pili pika kwa sekunde 30 ,weka mafuta kijiko 1 au 2 ipike mpaka itokee na rangi nzuri unayoipenda, itoe

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni