Mishamo Tz

Jumapili, 1 Oktoba 2017

Sababu Ya Daktari Bingwa Kushindwa kufanya Upasuaji Mtwara


Daktari bingwa wa masikio, koo na pua, Jonas Ndasika ameshindwa kufanya upasuaji kutokana na ukosefu wa vifaa hivyo katika Hospitali ya Rufaa ya Ligula mkoani Mtwara.

Akizungumza baada ya kumaliza utoaji wa huduma za madaktari bingwa ulioandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mganga Mfawidhi wa Ligula, Kariamel Wandi amesema utoaji wa huduma hizo umeonekana wa kusua sua kutokana na baadhi ya vifaa kukosekana na katika hospital hiyo.

Mganga Mfawidhi wa Ligula, Kariamel Wandi. 

“Daktari bingwa wa masikio, koo na pua ndiyo daktari pekee ambaye ameshindwa kufanya upasuaji kwa sababu hospitali yetu ya Ligula haina vifaa hivyo,” amesema.

“Vifaa vya masikio, koo na pua hakuna kabisa katika hospitali yetu na huduma hii haijawahi kutolewa  kama iliwahi kutolewa labda miaka ya nyuma.”

Mganga huyo ameomba Serikali kuhakikisha hospitali ambazo zipo pembezoni zinakuwa na vifaa pamoja na madaktari ili kuweza kufanya kazi wa ufanisi mzuri zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni