Mishamo Tz

Ijumaa, 6 Oktoba 2017

Kashata za Maziwa ya Unga

MAHITAJI

Maziwa ya unga kikombe 1 na nusu
Sukari kikombe 1 na robo
Maji kikombe 1 na nusu
Arki ya vanilla kijiko 1 cha kula
Rangi ya chakula kjk 1 cha kul(orange)
Mafuta ya kupikia vjk 2 vya kula

MATAYARISHO

1. Kwenye sufuria au pan tia maji na sukari , wacha ichemke

2. Ikianza kutoa mapovu mazito ( dakika 8 hadi 10) tia rangi , arki na mafuta ya kupikia , koroga kg wacha ichemke tena

3. Subiria tena kwa dakika 3 mpaka
5 au iwe nzito ukiigusa kwa vidole viwili ukiwachia ifanye kama uzi au mfano wa gundi

1. Tia maziwa ya unga koroga haraka haraka kwa dkk 1 au mpaka mchanganyiko uwe mzito

1. Pakaza mafuta sehem yako ya kukatia au trey , weka mchanganyiko wako, tumia mwiko,kijiko au kifimbo kuwekea sawa, wacha upoe na ukate shape unayopenda


Chef Mishamo Tz

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni