Chef Mishamo Tz
MAHITAJI
Unga wa ngano vikombe 2
Maziwa kikombe 1(ya uvugu vugu)
Sukari kijiko 1 cha chakula
Chumvi kiasi
Yai 1
Hamira kijiko 1 cha chakula
Arki ya vanilla kijiko 1 cha chai
Rangi ya orange kidogo(si lazima)
Siagi kijiko 1 cha chakula
Mafuta kwa ajili ya kuchomea
Sukari nusu kikombe au zaidi (kwa ajili ya kuweka juu)
MATAYARISHO
1. Tia maziwa ya uvugu vugu kwenye bakuli ,pamoja na sukari kijko 1,chumvi,hamira,yai,arki na rangi ya orange
2. Koroga vizuri wacha kwa dakika 2 hadi 3, na ufunue ukoroge tena
1. Tia unga wa ngano kidogo kidogo huku unachanganya mpaka unamaliza
4.tia siagi kijiko 1 cha chakula ,changanya ,unga utakua unanyata(kushikana na mikono) ila ukande kwa mkono au mixer mpaka unga uwe mlaini( pakaza mafuta mikono yako ili usigandie kwenye mikono)
1. Utie unga ulioukanda kwenye bakuli uliopaka mafuta ufunike wacha uumuke mara mbili zaidi yake
6.ukiumuka utoe uchanganye , pakaza unga sehem ya kukandia ,weka donge la unga na ulitie unga juu yake
1. Sukuma unga kwa kutumia kifimbo cha kusukumijuicepati, unga usiwe mwembamba sana wala mnene sana ( inch 10-12 ) kulingana na unene utakaopenda
8.tumia chombo chochote cha kukatia donut , donat cutter au hata glass na kifuniko
9. Pakaza unga trey au sehem ziweke ziumuke tena kama dakika 5 au 10
1. Teleka mafuta yapate kiasi na uchome donuts zako pande zote mbili ziwe na rangi ya yellow ya kukoza na uzitoe ,ziweke kwenye tishu zijichuje mafuta
11. Wacha zipoe
1. Zizungushie sukari ya kawaida nyeupe
Enjoy! Na chai au juice
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni