MAHITAJI
Unga wa ngano vikombe 2 na nusu
Tui zito la maji kikombe 1
iliki kijiko 1
Unga wa custard vijiko 3 vya chakula
Yai 1
Sukari vijiko 4 vya chakula
Mafuta ya kupikia kijiko 1 cha chakula
Hamira kijiko 1 cha chakula
MATAYARISHO
1.Kwenye bakuli tia tui na hamira koroga kidogo, tia Iliki ya unga,mafuta ya kupikia ,sukari na yai , koroga kidogo kuchanganya na uhakikishe hamira imeyayuka
1. Pembeni changanya unga wa ngano na custard powder
2. Anza kutia unga kwenye bakuli la kukandia lenye mchanganyiko wa hamira, mpaka donge likichanganyika ukande unga
4. Haakikisha unga ni mlaini na haugandi kwenye vidole
1. Pakaza bakuli mafuta uweke unga ufunike mpaka uumuke kiasi au mara mbili yake
1. Ugawe madonge 4 sawa na uyafanye duara
1. Pakaza unga kwenye sehem yako ya kusukumia sukuma donge moja moja duara ukate mara 2 kupata maandazi 4
1. Yapange sehem yaumuke
Teleka mafuta yakipata moto choma kwa moto wa kiasi , ukiwiva upande 1 geuza wa pile mpaka yapige flour ya light brown na yatoe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni