Mishamo Tz

Jumapili, 15 Oktoba 2017

mapishi ya mchemsho wa ndizi na Nyama

Mapishi ya Mchemsho wa ndizi na nyama

Mahitaji

Ndizi mbichi 6
Nyama ya ng'ombe (nusu kilo)
Viazi mviringo 2
Kitunguu swaum
Tangawizi
Kitunguu maji
Nyanya 1 kubwa
Mafuta (vegetable oil)
Chumvi
Limao
Pilipili

Matayarisho

Chemsha nyama na limao, kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa

Jumatano, 11 Oktoba 2017

Mapishi ya pilau ya nyama ya ng'ombe na salad

Mapishi ya Pilau ya nyama ya ng'ombe na kachumbari


Mahitaji


Mchele (rice vikombe 3)
Nyama ya ng'ombe (beef 1/2 kilo)
Viazi mbatata (potato 3)
Vitunguu maji (onions 3)
Kitunguu swaum (garlic cloves 4)
Tangawizi iliyosagwa (ginger kiasi)
Hiliki nzima (cardamon 4)
Karafuu (clove 4)
Pilipili mtama (blackpepper 4)
Amdalasini (cirnamon stick 1)
Binzari nyembamba nzima(cumin seeds 1/2 ya kijiko cha chai)
Binzari nyembamba ya kusaga (ground cumin 1 kijiko cha chai)
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)
Nyanya (fresh tomato 3)
Limao (lemon 1)
Pilipili (chilli 1)
Hoho (green pepper)


Matayarisho



Chemsha nyama na chumvi na nusu ya limao mpaka iive kisha weka pembeni. Baada ya hapo andaa vitu vya pilau kwa kuloweka mchele kwenye maji kwa muda wa dakika 10.Menya na kukatakata vitunguu na viazi kisha weka pembeni na pia chemsha maji ya moto na uweke pembeni. Baada ya hapo weka sufuri jikoni na tia mafuta kiasi . Yakisha pata moto tia vitunguu na uvikaange mpaka viwe vya rangi ya kahawia na kisha uitie nyama na ikaange mpaka ipate rangi ya bown pia. Baada ya hapo tia kitunguu swaum na tangawizi na uikoroge vizuri kisha iache ikaangike kwa muda wa dakika 2 kisha tia spice ambazo ni Binzari nyembamba ya unga, hiliki,karafuu, amdalasini na pilipili mtama na viazi. Baada ya hapo unatakiwa ugeuze geuze mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia mchele na ugeuzege mpaka uchanganyike na viungo. Baada ya hapo tia chumvi na maji ya kutosha na ukoroge vizuri kisha funika na uache uchemke katika moto wa wastani. Maji yakikaribia kukauka tia binzari nyembamba nzima na ufunike uache mpaka maji yakauke kabisa. maji yakisha kauka ugeuze na ufunike tena na uuache mpaka uive.
Baada ya hapo andaa kachumbali kwa  kukatakata vitunguu katika bakuli na kisha tia chumvi kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu. Baada ya hapo vioshe mpaka chumvi yote iishe. osha nyanya, Pilipili, hoho na kisha katakata slice nyembamba na uchanganye na vitunguu. Baada ya hapo tia chumvi, kamulia limao na uchanganye zote pamoja. Baada ya hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Tambi za sukari

Chef Mishamo

➡Mapishi ya Tambi za sukari

Mahitaji

Tambi (spaghetti 1/2 ya packet)
Mafuta (vegetable oil)
Sukari (sugar 1/2 kikombe cha chai)
Hiliki (cardamon 1/2 kijiko cha chai)
Chumvi (salt 1/2 kijiko cha chai)
Tui la nazi (coconut oil 1 kikombe cha chai)
Maji kiasi


Matayarisho

Tia mafuta kiasi kwenye sufuria kisha ibandike jikoni (katika moto wa wastani) yakisha pata moto kiasi tia tambi na uanze kuzikaanga kwa kuzigeuzageuza kila mara mpaka zitakapokuwa za yangi ya light brown. baada ya hapo ipua na umwage mafuta ya kwenye tambi (bakiza kidogo sana kwani usipofanya hivyo tambi zitakuwa na mafuta sana) Baada ya hapo zirudishe jikoni na kisha utie hiliki, chumvi, sukari, tui la nazi na maji kiasi. Zifunike kisha ziache zichemke mpaka maji yakauke. Baada ya hapo zigeuze na uzipike mpaka ziive. Nahapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Bagia Dengu

Mapishi ya Bagia dengu


Mahitaji
Unga wa dengu (gram flour 1/4 kilo)
Kitunguu kilichokatwa (onion 2)
Hoho (green pepper 1/2)
Pilipili iliokatwakatwa (scotch bonnet pepper 1/2)
Barking powder (1/4 ya kijiko cha chai)
Chumvi (salt)
Kitunguu swaum (garlic cloves 2)
Mafuta ya kukaangia (vegetable oil)
Binzari manjano (turmeric 1/4 ya kijiko cha chai)

Matayarisho

Changanya unga, chumvi, binzari, barking powder kwanza kisha weka maji kiasi na vitu vyote vilivyobakia (isipokuwa mafuta) na ukoroge vizuri kuhakikisha unga hauna madonge.Hakikisha unga hauwi mzito wala mwepesi sana. Kisha uache kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo choma bagia katika mafuta. Ukiwa unachoma hakikisha bagia zinakuja juu ya mafuta na hazigandi chini. Ikitokea zinaganda chini hapo itakuwa umekosea kitu. Pika mpaka ziwe za light brown kisha zitowe na uziweke katika kitchen towel ili zikauke mafuta na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kipika Mkate wa sinia

Chef
mishamo

Jinsi ya kupika Mkate wa sinia


Mahitaji



Unga wa mchele (rice flour 2 vikombe vya chai)
Sukari (sugar 3/4 ya kikombe cha chai)
Hamira (dried yeast 3/4 kijiko cha chakula)
Hiliki (cardamon powder 1/2 kijiko cha chai)
Ute wa yai 1(egg white)
Tui la nazi (coconut milk kikombe 1 na 1/2 cha chai)
Mafuta (vegetable oil)


Matayarisho


Changanya unga wa mchele, hamira, hiliki na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastic kisha koroga vizuri. Ufunike na uwache katika sehemu ya joto mpaka uumuke.(ambayo inaweza kuchukua kama dakika 30-45. Ukisha umuka tia sukari na ute wa yai kisha ukoroge vizuri. Baada ya hapo washa oven katika moto wa 200°C kisha chukua chombo cha kuokea na ukipake mafuta na umimine mchanganyiko. Kisha utie katika oven na uoke kwa muda wa dakika 40. Hakikisha unaiva na kuwa rangi yabrown juu na chini. Na hapo mkate utakuwa tayari.

Mapishi Ya Biriani

Mapishi ya Biriani

Mahitaji

Mchele (rice 1/2 kilo)
Nyama (beef 1/2 kilo)
Vitunguu (onion 2)
Kitunguu swaum (garlic 1 kijiko cha chai)
Tangawizi (ginger 1 kijiko cha chai)
Maziwa mgando (yogurt 1 kikombe cha chai)
Hiliki nzima (cardamon 6)
Amdalasini nzima (cinamon stick 2)
Karafuu nzima (cloves 6)
Pilipili mtama nzima (black pepper 8)
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Binzari manjano (turmaric 1/2 kijiko cha chai)
Binzari nyembamba nzima (cumin 1/4 kijiko cha chai)
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia nyama na uikaange kwa muda wa dakika 10. baada ya hapo tia tangawizi, kitunguu swaum, hiliki(4), amdalasini (1), karafuu (4), pilipili mtama (5), Curry powder, binzari manjano, binzari nyembamba na chumvi. Kisha koroga. Baada ya hapo tia yogurt na uipike mpaka ikauke kisha tia maji kidogo, funika na upunguze moto na uache ichemke kwa muda wa nusu saa.Baada ya hapo nyama itakuwa imeiva na mchuzi kubakia kidogo.Kwahiyo itatakiwa kuiipua.
Loweka mchele kwa dakika 10. kisha chemsha maji mengi kidogo katika sufuria kubwa. baada ya hapo tia hiliki (2) amdalamsini (1) karafuu(2) pilipili mtama (3) chumvi na mafuta kiasi. acha ichemke kidogo kisha tia mchele.Hakikisha maji yameufunika mchele kabisa na uuache uchemke kwa muda wa dakika 8 tu (kwani hautakiwi kuiva kabisa) kisha uipue na uchuje maji yote katika chujio. baada ya hapo chukua sufuria ya kuokea (baking pot kama unayoiona kweye picha) Kisha weka wali nusu na uusambaze sawia kisha weka mchuzi nyama na mchuzi wake pia utandaze na umalizie kwa kuweka leya ya wali uliobakia. Baada ya hapo ufunike na uweke kwenye oven kwenye moto wa 200°C kwa muda wa nusu saa .na baada ya hapo biriani litakuwa tayari kwa kuliwa.






Shukrani

Asante sana Sir phabian kwa recipe yako. Nimeijaribu na biriani limetoka bomba. Nikaona ni vizuri kuipublish recipe hii ili na wadau wengine wafaidike na namna nyingine ya kupika biriani. Na kama kuna wadau wengine wana recipe zao na wangependa kushare nasi, si vibaya kama watanitumia nami nitazipublish kwa moyo mkunjufu.
Asante sana.

Mapishi ya Pasta za cream na uyoga

Chef
Inno Mishamo

Mapishi ya Pasta za cream na uyoga

Mahitaji

Pasta (2 na 1/2 vikombe vya chai)
Uyoga (mashroom 2 vikombe vya chai)
Cream (1 kikombe cha chai)
Mafuta (vegetable oil)
Kitunguu (onion 1)
Chumvi
Majani ya basil (dried basil leaves 1/2 kijiko cha chai)

Matayarisho


Chemsha maji ya kutosha kisha tia chumvi na mafuta kidogo katika hayo maji na baadae tia pasta na uzichemshe mpaka ziive kisha uzichuje maji na uziweka pembeni. Baada ya hapo weka mafuta kidogo katika sufuria kisha tia uyoga uliokatwa na uupike mpaka uive. Baada ya hapo tia majani ya basil, chumvi na cream kisha acha ichemke kisha weka vitunguu na upike kwa muda wa dakika 4 kisha malizia kwa kutia pasta. Zichanganye vizuri na mchanganyiko wote kisha zipike kwa muda wa dakika 5. Na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Unaweza kupika nyama ya kuku (chiken breast) iliyokatwa vipande vidogo vidogo kama saizi na shape ya pasta. Vizuri kuikaanga pembeni mpaka iwe brown na kuiva alafu kuimix kwenye chakula baada ya uyoga na vitunguu kuiva alafu unamix cream kumalizia mapishi.

Mapishi ya wali na kuku wa kienyeji

Chef Inno Mishamo

Mapishi ya Wali na kuku wa kienyeji

Mahitaji

Kuku wa kienyeji (boiler chicken 1)
Mchele (rice 1/2 kilo)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1)
Vitunguu (onion 2)
Vitunguu swaum (garlic cloves 6)
Tangawizi (ginger)
Carry powder
Binzari ya njano (Turmaric 1/2)
Njegere(peas 1/2kikombe)
Carrot iliyokwanguliwa 1
Limao (lemon 1)
Bilinganya (aubergine 1)
Chumvi
Pilipili (scotch bonnet pepper)
Mafuta (vegetable oil)


Matayarisho


Loweka mchele kwa muda wa dakika 10 na uchuje maji yote kisha chemsha maji ya moto na uweke pembeni. Kisha tia mafuta kiasi katika sufuria na ukaange vitunguu, carrot na njegere pamoja. kwa muda wa dakika 5 baada ya hapo tia turmaric na chumvi. pika kwa muda wa dakika 5 na utie mchele na maji ya moto kiasi funika na upike mpaka uive.
Chemsha kuku pamoja na limao, chumvi, kitunguu swaum na tangawizi mpaka aive kisha mweke pembeni. Saga pamoja kitunguu,kitunguu swaum, tangawizi na nyanya. Kisha bandika jikoni na uache uchemke bila mafuta mpaka maji ya kauke.Baada ya hapo tia chumvi, mafuta ,curry powder, bilinganya na kuku. Kaanga pamoja kwa muda kisha tia maji au supu ya kuku kwa kukadiria mchuzi uutakao. Acha uchemke mpaka mabilinganya yaive na hapo mchuzi utakuwa tayari kuseviwa na wali

Mapishi ya potato Wedged na Samaki wa kuoka

Mapishi ya Potato wedges na samaki wa kuoka

Mahitaji

Viazi ulaya (baking potato 5 vya wastani)
Parprika 1 kijiko cha chai
Pilipili mtama ilyosagwa (ground black pepper 1 kijiko cha chai
Kitunguu swaum cha unga (garlic powder 1 kijiko cha chai)
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)
Marination za samaki (angalia kwenye recipe ya samaki ya nyuma)

Matayarisho

Osha viazi na maganda yake kisha vikaushe na uvikate vipande vya wastani. Kwa kila kiazi toa vipande

6. Kisha vitie kwenye bakuli na utie parpika, pilipili mtama ya unga, kitunguu swaum cha unga, chumvi na mafuta kama vijiko 2 vya chakula. Changanya pamoja na kisha uvibake katika oven kwa muda wa dakika 25. Hakikisha vinakuwa rangi ya brown. Vikisha iva vitoe.
Wamarinate samaki, na uwaoke kisha wasevu na potato wedges tayari kwa kuliwa
(Jinsi ya kupika samaki, angalia katika recipe za nyuma)

Mapishi Ya wali na stuffed Pepper

Mapishi ya Wali na stuffed pepper

Mahitaji

Pilipili hoho (Red pepper 3)
Cougette 1
Kitunguu (onion 1)
Uyoga (mashroom 1 kikombe cha chai)
Carrot 1
Nyanya (fresh tomato 1)
Nyanya ya kopo iliyosagwa (tomato paste 3 vijiko vya chai)
Giligilani (fresh coriander)
Binzari manjano (Turmaric 1/2 ya kijiko cha chai)
Curry powder 1/2 ya kijiko cha chai
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Kata hoho kati na utoe moyo wake kisha ziweke pembeni, Kisha katakata cougette, kitunguu, uyoga, carrot, nyanya katika vipande vidogo vidogo, Weka sufuria jikoni na uanze kupika uyoga kwa muda wa dakika 5, kisha weka curry powder, turmaric na chumvi na kaanga kidogo kisha weka vegetable zilizobakia pamoja na nyanya ya kusaga pamoja na giligilani. Zikaange kwa muda wa dakika 5 kisha zitie kwenye hoho na kisha uzibake kwa muda wa dakika 20 na hapo zitakuwa tayari kuseviwa na wali.
Wali: angalia katika recipe zilizopita

Jinsi ya Kupika Kalmati

Chef
Inno Mishamo

Jinsi ya Kupika Kalmati

Mahitaji

Unga wa ngano (self risen flour 2 vikombe vya chai)
Hamira (yeast kijiko 1 cha chai)
Sukari (sugar 2 vikombe vya chai)
Hiliki (cardamon 1/4 ya kijiko cha chai)
Maji kikombe1 na 1/2
Mafuta

Matayarisho

Changanya unga, hamira, maji na mafuta kijiko 1. Koroga vizuri mpaka upate uji mzito usiokuwa na madoge Baada ya hapo uache uumuke kisha zichome kalmati katika moto wa wastani. Baada ya hapo tia sukari, hiliki na maji 1/2 kikombe katika sufuria na ichemshe uku unakoroga mpaka iwe tayari.(ukitaka kujua kama iko tayari chovya mwiko kisha gusa na vidole utaona iko kama nta au gundi) Baada ya hapo tia kalmati na uzichange pamoja mpaka zikolee kisha zitoe na uziache mpaka zipoe tayari kwa kuliwa.

Jollof rice

Jollof rice (wali wa ki-west Africa)

Mahitaji

Mchele (rice vikombe 2 na 1/2)
Vitunguu (onion 2)
Nyanya ya kopo (tin tomato kopo 1)
Tangawizi (ginger paste kijiko 1 cha chakula)
Kitunguu swaum (garlic paste kijiko 1 cha chakula)
Paprika (kijiko 1 na 1/2 cha cha chai)
Pilipil (scotch bonnet pepper 1)
Curry powder (kijiko 1 cha chai)
Maggi cubes 3(unaweza kutumia yenye ladha ya chicken, beef au vegetable. Inategemea unasevu na mchuzi wa aina gani)
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Loweka mchele kwa muda wa dakika 10.Katakata vitunguu kisha weka pembeni, saga pamoja nyanya ya kopo,pilipili, tangawizi na kitunguu swaum kisha weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu vikiiva tia curry powder, maggi cubes, chumvi na paprika na uchanganye vizuri. Kisha tia mchanganyiko wa nyanya na uupike mpaka uive. Baada ya hapo tia mchele na maji na uupike mpaka ukaribie kuiva kisha ugeuze na umalizie kwa kutia njegere na umalizie kuupika mpaka uive. baada ya hapo utakuwa tayari kuseviwa na mboga yoyote kama kuku, nyama, samaki au assorted meat (Mchanganyiko wa utumbo, makongoro na nyama), Hapo mimi nili-save na mchuzi wa kuku wa kienyeji

Jinsi ya Kupika scones

Chef
Inno Mishamo

Jinsi ya Kupika Scones

Mahitaji

Unga wa ngano (self risen flour 2 vikombe vya chai)
Sukari (sugar 1/2 kijiko cha chakula)
Chumvi (salt 1/2 kijiko cha chai)
Hamira (yeast 1/2 kijiko cha chakula)
Baking powder 1/2 kijiko cha chai
Siagi (butter 1/4 ya kikombe cha chai)
Maziwa (fresh milk 3/4 ya kikombe cha chai)(unaweza kutumia maji badala ya maziwa)

Matayarisho

Pasha maziwa yawe ya uvuguvugu kisha weka pembeni, pia yeyusha siagi na uweke pembeni.Baada ya hapo tia kila kitu kwenye bakuli la kukandia kasoro maziwa, na uchanganye vizuri kisha tia maziwa kidogo kidogo katika mchanganyiko huo kisha ukande. Ukimaliza uweke kwenye sehemu ya joto na uache uumuke. Ukisha umuka utawanyishe katika madonge saba Kisha .pakaza mafuta au siagi katika chombo cha kuokea kisha yapange hayo madonge katika hicho chombo na uyaache yaumuke tena (kwa mara ya pili). Baada ya hapo pakaza mafuta juu ya hayo madonge na uyaoke (bake) katika oven (moto 200°C ) kwa muda wa dakika 25 na hapo scones zitakuwa tayari

Mapishi ya maharage

Mapishi ya Maharage

Mahitaji

Maharage (beans 2 vikombe vya chai)
Nazi (coconut milk kiasi)
Vitunguu maji (onion 1kikubwa)
Nyanya (fresh tomato 1)
Kitunguu swaum (garlic paste 1/4 kijiko cha chai)
Chumvi (salt kiasi)
Curry powder 1 kijiko cha chai
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Chemsha maharage mpaka yaive kisha yaweke pembeni. Kaanga vitunguu maji na mafuta mpaka vianze kuwa vya brown kisha weka kitunguu swaum,nyanya na curry powder. kaanga mpaka nyanya iive kisha tia maharage na chumvi kiasi. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri. Baada ya hapo tia tui la nazi na ukoroge vizuri na uache lichemke mpaka liive. Baada ya hapo ipua na maharage yatakuwa tayari kwa kuliwa

Mapishi Ya sambusa za nyama

Chef
Inno Mishamo

Mapishi ya Sambusa za nyama

Mahitaji

Nyama ya kusaga (minced beef 1/4 kilo)

Vitunguu maji

vilivyokatwakatwa(diced onion)
vikubwa )
Kitunguu swaum/ tangawizi (garlic and ginger paste 1 kijiko cha chakula)
Chumvi (salt)
Pilipili iliyokatwakatwa (scotch bonnet 1)
Limao (lemon 1/2)
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Cinnamon powder 1/4 kijiko cha chai
Coriander powder 1/4 kijiko cha chai
Cumin powder 1/4 kijiko cha chai

Unga wa ngano (all purpose flour kidogo)

•Manda za kufungia (spring roll pastry)

•Giligilani (fresh coriander kiasi)
Mafuta ya kukaangia

Matayarisho

Changanya nyama na limao, chumvi, pilipili,kitunguu swaum, tangawizi na spice zote, kisha pika katika moto wa kawaida mpaka nyama iive na maji yote yakauke. Baada ya hapo kabla hujaipua nyama tia vitunguu na giligilani na uvipike pamoja kwa muda wa dakika 2 na uipue weka pembeni na uache viipoe. Baada ya hapo tia unga kidogo katika bakuli nauchanganye na maji kidogo kupata uji mzito kwa ajili ya kugundishia manda. Baada ya hapo tia nyama katika manda na kisha zifunge kwa kugundishia na unga wa ngano.Ukisha maliza kuzifunga zote zikaange mpaka ziwe za brown na uzitoe. Na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Tandoori Chicken

Mapishi ya Tandoori chicken (kuku)

Mahitaji

Kuku mzima 1 ( A whole chicken)(mimi huwa natumia baby chiken)
Kitunguu swaum/tangawizi (garlic & ginger paste) 1 kijiko cha chai
Maziwa ya mgando (plain yogurt )1 kikombe cha chai
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Garam masala 1/2 kijiko cha chai
Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
Cumin powder 1/2 kijiko cha chai
Chilli powder 1/2 kijiko cha chai
Limao (lemon)1/2
Chumvi (salt ) kiasi
Rangi ya chakula nyekundu (food colour) few drops
Mafuta ya kupikia (vegetable oil) vijiko 2 vya chakula

Matayarisho

Katakata kuku katika vipande vya kawaida kisha umuoshe na umkaushe maji kwa kutumia kitchen towel. Baada ya hapo muweke katika bakuli kubwa na uanze kutia limao na spice zote kasoro mafuta, yogurt na rangi ya chakula. Changanya spice na kuku mpaka vikolee vizuri. Baada ya hapo changanya yogurt na rangi ya chakula pembeni na kisha umwagie katika kuku na uchanganye tena vizuri. Baada ya hapo malizia kwa kutia mafuta na uchanganye vizuri kisha funika na uweke katika friji kwa muda wa masaa 3 ili kuku aingie viungo.
Baada ya hapo muoke kuku wako katika oven kwa muda wa nusu saa katika moto wa 200°C.Baada ya hapo kuku wako atakuwa tayari kwa kuliwa.
Mtanisamehe picha imekaa upande maana niliipiga vibaya

Mapishi ya Chicken Satay

Chef
Mishamo

Mapishi ya Chicken Satay

Mahitaji

Kidali cha kuku 1 (chicken breast)
Kitunguu maji 1/2 (onion)
Kitunguu swaum/tangawizi (garlic and ginger paste) 1 kijiko cha chai
Limao ( lemon)1/4 kijiko cha chai
Curry powder 1/4 kijiko cha chai
Pilipili ya unga kidogo (Chilli powder)
Coriander powder 1/4 kijiko cha chai
Soy sauce 1kijiko cha chai
Mafuta 2 vijiko vya chai.
Chumvi kiasi (salt)
Vijiti vya mishkaki

Matayarisho

Osha kidali kisha kikaushe maji na kitchen towel na ukate vipande(cubes) vidogodogo na uweke pembeni. Baada ya hapo changanya vitu vyote (kasoro vijiti )na utie vimaji kidogo kisha visage katika breda kupata paste nzito. Baada ya hapo changanya hiyo paste na kuku na uache zimarinate kwa muda wa saa moja. Baada ya hapo zitunge kuku katika vijiti vya kuchomea na uzichome katika oven mpaka ziive (inaweza kuchukua kama dakika 10). Baada ya hapo chicke

Mapishi ya Aloo Vada

Chef
Inno Mishamo

Mapishi ya Aloo vada

Mahitaji

Viazi ulaya vya wastani (Potato) 5
Kitunguu maji (onion) 1/2
Kitunguu swaum na tangawizi( ginger and garlic paste) 1 kijiko cha chai
Unga wa dengu (garam flour) 1/2 kikombe cha chai
Giligilani iliyokatwakatwa (fresh chopped coriander) kiasi
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Turmaric 1/4 kijiko cha cha chai
Chilli powder 1/4 ya kijiko cha chai
Chumvi (salt) kiasi
Mafuta ya kukaangia (veg oil)

Matayarisho

Chemsha viazi mpaka vilainike kisha viponde na uviweke pembeni. Baada ya hapo katakata kitunguu maji vipande vidogovidogo na uvitie katika viazi,kisha malizia kwa kutia vitu vyote vilivyobaki(kasoro mafuta ya kukaangia).Baada ya hapo changanya vizuri kisha utengeneze shape uipendayo (inaweza kuwa maduara au ring) Baada ya hapo zikaange katika moto wa wastani mpaka ziive. Na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya half Cake

Chef
Inno Mishamo

Mapishi ya Half cake (Keki)

Mahitaji

Unga wa ngano (self risen flour) kikombe 1na 1/2
Sukari (sugar) 1/4 kikombe
Barking powder 1/2 kijiko cha chai
Magadi soda (bicarbonate soda) 1 kijiko cha chai
Mafuta 2 vijiko vya chai
Mafuta ya kukaangia
Maji ya uvuguvugu kiasi

Matayarisho

Changanya unga na vitu vyote (kasoro mafuta ya kuchomea) kisha ukande (hakikisha unakuwa mgumu) Baada ya hapo sukuma na ukate shape uipendayo (hakikisha unakata vipande vinene kiasi na sio kama mandazi) Baada ya hapo ziweke sehemu yenye joto na uache ziumuke. Zikisha umuka zikaange katika moto mdogo ili ziive mpaka ndani. Zikisha iva zitoe na uziweke katika kitchen towel ili zichuje mafuta. Ziache zipoe na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Jumanne, 10 Oktoba 2017

Mapishi ya kofta curry

Mapishi ya Kofta curry

Mahitaji

Vitu vya kofta
Nyama ya kusaga (minced beef) 1/4 kilo
Yai (egg) 1
Kitunguu maji (chopped onion) 1
Kitunguu swaum/ tangawizi (ginger and garlic paste) 1 kijiko cha chakula
Garam masala powder 1 kijiko cha chai
Pilipili ya unga (chilli powder) 1/2 ya kijiko cha chai
Limao (lemon) 1/2
Breadcrumbs 3 vijiko vya chakula
Chumvi (salt)
Vitu vya curry
Tui la nazi (coconut milk) kopo 1
Nyanya (fresh tomato) 2
Kitunguu (onion) 1
Kitunguu swaum/tangawizi (ginger and garlic paste) 1 kijiko cha chai
Curry powder 1 kijiko cha chai
Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
Turmaric 1/2 ya kijiko cha chai
Chumvi (salt)
Mafuta (veg oil) kiasi
Giligilani (coriander)

Matayarisho

Changanya nyama na vitu vyake vyote kisha iache kwa muda wa 1/2 saa ili iingie viungo. Baada ya hapo tengeneza maduara na uyapange kwenye baking tray kisha zichome kwenye oven mpaka ziive. Baada ya hapo saga pamoja nyanya, kitunguu, swaum na tangawizi. kisha vitie kwenye sufuria na upike mpaka maji yote yakauke, kisha weka mafuta kidogo, chumvi na spices zote koroga mpaka vichanganyike vizuri kisha tia tui la nazi. Liache lichemke mpaka libakie kidogo na umalizie kwa kutia kofta. Zichanganye vizuri na huo mchuzi kisha ziache zichemke kidogo na uipue. Malizia kwa ku garnish na coriander na hapo kofta curry yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kula kwa wali, ugali, viazi au chapati.

Jinsi ya kupika Mkate

Chef
Inno Mishamo

Jinsi ya kupika Mkate

Mahitaji

Unga wa ngano ( self risen flour) kikombe 1 na 1/2
Hamira (yeast) 1 kijiko cha chai
Sukari (sugar) 1 kijiko cha chakula
Chumvi (salt) 1/2 kijiko cha chai
Siagi iliyoyeyushwa (melted butter) 1 kijiko cha chakula
Maji ya uvuguvugu ( warm water) kiasi

Matayarisho

Changanya vitu vyote katika bakuli kubwa kisha aanza kukanda mpaka upate donge laini.Baada ya hapo liweke hilo donge kwenye bakuli la plastic na weke katika sehemu yenye joto ili unga uumuke. Hakikisha unga unaumuka zaidi (yani unaji double size) unaweza kuchukua kama saa 1 na nusu hivi. Baada  ya hapo ukande tena na uache uumuke tena kwa mara ya pili, Ukisha umuka pakaza butter katika baking tin (chombo cha kuokea) na upakaze mkate butter kwa juu,kisha uoke katika oven kwa muda wa dakika 30 (katika moto wa 200C) (hakikisha juu na chini unakuwa wa brown Na hapo mkate wako utakuwa tayari

Mapishi ya Samaki wa kuokwa

Mapishi ya Samaki wa kuokwa

Mahitaji


Mackerel 2
Kitunguu swaum na tangawizi (ginger and garlic paste) 1 kijiko cha cha kula
Pilipili iliyo katwakatwa (chopped scotch bonnet ) 1/2
Limao (lemon) 1/2
Chumvi (salt) kiasi
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
Mafuta 1 kijiko cha chai

Matayarisho

Safisha samaki kisha wakaushe maji ( ukipenda unaweza kuwakata kati au ukawapika wazima) Baada ya hapo wakate mistari kila upande ( ili spaces ziweze kuingia ndani) kisha waweke kwenye bakuli na utie spice zote. Wachanganye vizuri kisha waweke frijini na uwaache wamarinate kwa muda wa masaa 3. Baada ya hapo washa oven kisha wapakaze mafuta na uwafunge kwenye foil na uwatie kwenye oven kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo fungua foil na uwaache kwenye oven kwa muda wa dakika 10 ili wapate kukauka kidogo. Na hapo watakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuwala kwa kitu chochote upendacho.

Mapishi ya kababu

Chef
Inno Mishamo

Mapishi ya Kababu (Meatballs)

Mahitaji

Nyama ya kusaga (minced beef) 1/2 kilo
Kitunguu kikubwa (large onion) 1
Kitunguu swaum/ tangawizi (ginger/garlic paste) 1 kijiko cha chakula
Chenga za mkate (Breadcrambs) 3 vijiko vya chakula
Yai (egg) 1
Curry powder 1 kijiko cha chai
Turmaric 1/2 kijiko cha chai
Pilipili ya unga (chilli powder 1/2 kijiko cha chai
Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
Giligilani (fresh chopped coriander)
Limao (lemon) 1/2
Chumvi
Mafuta ya kukaangia

Matayarisho

Changanya vitu vyote (kasoro mafuta ) katika bakuli hakikisha mchanganyiko wako umechanganyika vizuri, kisha tengeneza maduara ya wastani na uyahifadhi frijini kwa muda wa masaa 4 (au unaweza kuziacha zimarinate kwa usiku mzima) Baada ya hapo zikaange kwenye mafuta mpakaziive naziwe rangi ya brown. Kisha ziipue na uziweke kwenye kitchen towel ili zichuje mafuta na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Pia unaweza kuzibake katika oven kama hutaki kuzikaanga.

Mapishi Ya Viazi ulaya

Chef Mishamo

Mapishi ya Viazi Ulaya

Mahitaji

Viazi mbatata (potato) 1 kilo
Vitunguu (onion) 2
Kitunguu swaum (garlic paste) 1 kijiko cha chai
Carrot zilizokwanguliwa (grated carrots) 2
Hoho jekundu lilokatwakatwa (chopped red pepper) 1
Hoho la kijani lilokatwakatwa (chopped green pepper) 1
Curry powder 1 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia kiasi
Chumvi (salt)
Fresh coriander kiasi

Matayarisho

Katakata viazi katika vipande vya wastani kisha vichemshe na chumvi mpaka viive kisha viweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu kidogo (visiwe vya brown) kisha tia kitunguu swaum, hoho zote na curry powder. Changanya vizuri na uzipike kwa dakika 2 kisha tia viazi,carrot na chumvi kidogo na vimaji kidogo uchanganye vizuri na upunguze moto na kisha vipike kwa muda wa dakika kumi. Baada ya hapo malizia kwa kutia coriander na uipue. Na hapo viazi vyako vitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi Ya sponge Keki

Chef Mishamo

Mapishi ya Sponge keki

Kwa walioniomba recipe ya sponge cake hiyo ni kwa ajili yenu.

Mahitaji

Unga wa ngano (self risen flour) 100g
Sukari (sugar) 100g
Siagi isiyokuwa na chumvi (unsalted butter) 100g
Mayai (eggs) 2
Vanila 1 kijiko cha chai
Chumvi pinch
Warm water 3 vijiko vya chakula

Matayarisho

Kwanza washa oven moto wa 200 C. Baada ya hapo saga butter na sukari mpaka viwe laini kisha tia mayai na uendelee kusaga mpaka vichanganyike vizuri kisha tia unga, vanila, chumvi na na maji na usage mpaka upate uji usiokuwa mzito sana au mwepesi sana. Baada ya hapo utie kwenye baking tin na u bake kwa muda wa dakika 25 na mpaka cake yako iive yani juu na chini iwe ya brown na ukidumbukiza kijiti katikati kinatoka kikiwa clean. Baada ya hapo itoe kwenye tin na uiache ipoe. Ikisha poa itakuwa tayari kwa kuliwa.

Broccoli soup

Chef Mishamo

Broccoli soup

Mahitaji

Broccoli Kichane 1
Viazi (potato) 2 vya wastani
Supu (chicken or vegetable broth) 2 vikombe
Kitunguu (onion) 1 kikubwa
Mafuta ya kupikia 1 kijiko cha chakula
Chumvi (salt) kiasi
Pilipili 1/4
Limao 1/4

Matayarisho

Katakata broccoli, viazi na kitunguu katika vipande vya wastani kisha viweke katika sufuria ya kuchemshia na utie maji kidogo na chumvi. Chemsha mpaka viazi na broccoli viive kisha tia supu, pilipili, mafuta na ukamulie limao baada ya hapo chemsha tena kwa dakika 5 na baada ya hapo isage na itakuwa tayari kwa kuseviwa

Mapishi ya wali wa kukaanga

Chef Mishamo

Mapishi ya Wali wakukaanga

Mahitaji

Mchele (Basmati rice) 1 kilo
Vitunguu (chopped onion) 2 vikubwa
Garlic powder 1/2 kijiko cha chai
Njegere (peas) 1 kikombe
Turmaric 1/2 kijiko cha chai
Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
Cumin seeds 1/2 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia 2 vijiko vya chakula
Chumvi kiasi

Matayarisho

Osha kisha loweka mchele kwa muda wa dakika 5 na kisha uchuje maji na uweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown na kisha tia spices zote.Zikaange kwa muda wa dakika 3 kisha tia mchele na uchanganye vizuri na spice.Ukaange mchele pamoja na spice uku ukiwa unageuzageuza kwa muda wa dakika 5. Baada ya hapo tia maji ya moto(kiasi ya kuivisha wali) na chumvi kisha ufunike. Upike mpaka uive kisha malizia kwa kutia njegere na uchanganye vizuri baada ya dakika 2 uipue utakuwa tayari kwa kuliwa.Unaweza kuula kwa mboga yoyote uipendayo

Mapishi Ya Mlenda Wa Bamia na nyanya Chungu

Chef Mishamo

Mapishi ya Mlenda wa bamia na nyanya chungu

Mahitaji

Bamia (okra) 20
Nyanya chungu (garden eggs) 5
Magadi soda (Bicabonate soda) 1/4 ya kijiko cha chai
Nyanya (fresh tomato) 1
Chumvi (salt) kidogo
Pilipili 1/4

Matayarisho

Osha bamia, nyanya chungu na nyanya kisha vikatekate katika vipande vidogovidogo. Baada ya hapo vitie kwenye sufuria na vitu vyote vilivyobakia na kisha tia maji kidogo.Chemsha mpaka bamia na nyanya chungu ziive na vimaji vibakie kidogo sana. Baada ya hapo ziponde na mwiko kidogo kisha zikoroge na uipue na mlenda utakuwa tayari kwa kuliwa na ugali.

Mapishi ya Maini Ya Ngo'mbe

Mapishi ya Maini ya ng'ombe

Mahitaji

Maini (Cow liver) 1/4 kilo
Vitunguu (chopped onion) 2
Nyanya (chopped tomato) 1
Kitunguu swaum/tangawizi (ginger /garlic paste) 1 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia
Chumvi
Coriander
Curry powder 1 kijiko cha chai
Limao (lemon) 1/4

Pilipili (scotch bonnet ) 1

Matayarisho

Safisha maini na ukate vipande vidogovidogo na uweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu kidogo(visiwe vya brown) kisha tia ginger/ garlic paste,carry powder kaanga kidogo kisha tia nyanya. Kaanga nyanya mpaka zitoe mafuta kisha tia chumvi, pilipili na vimaji kidogo. Acha vichemke kidogo kisha tia maini na uyapike mpaka yaive. Malizia kwa kukamulia limao na kutia coriander kisha ipua na hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa

Mapishi Ya Chapati za Maji za vitunguu

Chef Mishamo

Mapishi ya Chapati za maji za vitunguu

Mahitaji

Unga wa ngano (plain flour) 1/4
Kitunguu kikubwa (chopped/slice onion) 1
Yai (egg) 1
Chumvi (salt)
Mafuta (cooking oil)

Matayarisho

Tia unga, chumvi na maji kiasi katika bakuli kisha koroga mpaka madonge yote yaondoke. Baada ya hapo tia yai na vitunguu kisha koroga tena mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. baada ya hapo choma chapati zako kama kawaida (jinsi ya kuchoma unaweza kuangalia kwenye recipe yangu ya chapati za maji katika older posts) na baada ya hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Chips

Chips (homemade)

Mahitaji

Viazi (potato) 1/2 kilo
Mafuta ya kukaangia (veg oil)
Chumvi

Matayarisho

Menya viazi kisha vioshe na vikaushe maji yote kwa kutumia kitchen towel.Baada ya hapo katakata katika shape ya chips uzipendazo either nyembamba au nene kisha zikaushe tena maji na uzitie chumvi. Baada ya kuzitia chumvi tu zitie kwenye mafuta ya kukaangia straightaway (hakikisha mafuta yasiwe ya moto sana kwani utazibabua) Zipike upande mmoja ukiiva geuza upande wa pili. Baada ya hapo endelea kuzipika uku ukiwa unazigeuzageuza mpaka kwa nje ziwe light brown na crisps.Baada ya hapo zitoe na uziweke kwenye kitchen towel ili zichuje mafuta na zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi Ya Kupika Fish Cakes

Jinsi ya kupika Fish cakes

Mahitaji

Fish fillet (steki ya samaki isiyokuwa na mifupa) kipande 1 kikubwa
Viazi (potato) 6 vya wastani
Kitunguu (onion) 1 kikubwa
Tangawizi na swaum (garlic and ginger paste) 1 kijiko cha cha chai
Breadcrumbs kiasi
Mayai (eggs) 2
Limao (lemon) 1/2
Chumvi (salt) kiasi
Pilipili (scotch bonnet chilli) 1/4
Curry powder 1/2 cha chai
Coriander powder 1/4 kijiko cha chai
Turmaric 1/4 kijiko cha chai
Fresh chopped coriander kiasi.
Mafuta ya kukaangia

Matayarisho

Chemsha viazi na chumvi kidogo kisha viponde na uviweke pembeni vipoe.Katakata samaki vipande kisha mtie kwenye sufuria pamoja na tangawizi, swaum, limao na chumvi. Mchemshe kidogo(hakikisha maji yote yanakauka) kisha mponde na uma (folk) baada ya hapo tia spice zote,pilipili na vitunguu vilivyokatwa vidogovidogo na uvipike pamoja na samaki kwa muda wa dk 3. Baada ya hapo tia coriander na kamulia limao kisha viweke pembeni. Baada ya hapo changanya viazi pamoja na mchanganyiko wa samaki kisha tengeneza maduara ya wastani. Baada ya hapo piga mayai ktk bakuli na chumvi kidogo.Bandika jikoni mafuta ya kukaangia ktk fry pan yawe kidogo tu (shallow fry) yakisha pata moto kiasi chukua madonge yako kisha yachovye ktk mayai na umalizie ktk breadcrumbs kisha zikaange ktk mafuta. Baada ya hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa

Mapishi ya filigisi za Kuku

Chef Mishamo

Mapishi ya Filigisi za kuku

Mahitaji

Filigisi (chicken gizzard) 1/2 kilo
Carrot iliyokwanguliwa 1
Nyanya 1/2 kopo
Vitunguu maji 1 kikubwa
Tangawizi/swaum 1 kijiko cha chai
Hoho 1 iliyokatwakatwa
Limao 1/2
Chumvi
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Turmaric 1/2 kijiko cha chai
Chilli powder 1/4 kijiko cha chai
Mafuta
Chopped coriander

Matayarisho

Safisha filigisi kisha zikate vipande vidogo vidogo.Zichemshe pamoja na chumvi, limao na nusu ya tangawizi na swaum mpaka ziive (hakikisha unabakiza supu kidogo). Baada ya hapo kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia tangawizi na swaum iliyobakia na kaanga kidogo kisha tia nyanya. Zipike mpaka ziive kisha tia spice zote pamoja na chilli. Zipike kidogo kisha tia filigisi (bila supu kwanza) Zichanganye vizuri na uzipike kidogo. Baada ya hapo tia carrot na hoho na supu iliyobakia. Vipike pamoja mpaka viive na supu ibakie kidogo sana. Malizia kwa kutia coriander na uipue na hapo firigisi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Potato And Fish Casserole

Potato and fish casserole

Mahitaji

Viazi (potato) 1/2 kilo
Fillet ya samaki isiyokuwa na mifupa 1 kubwa kiasi
Carrot 1
Maziwa kikombe 1 na 1/2
Unga wa ngano 2 vijiko vya chakula
Kitunguu maji 1 kikubwa
Cheese iliyokwanguliwa 1/4 kikombe
Butter 1 kijiko cha chakula
Curry powder 1/2 kijiko chai
Turmaric 1/4 kijiko cha chai
Tangawizi/ swaum 1/2 kijiko cha chai
Chumvi

Matayarisho

Katakata viazi na carrot katika cubes ndogondgo kisha tia chumvi kidogo sana na uvichemshe kidogo vikikaribia kuiva viipue na uviweke pembeni. Katika sufuria nyingine tia butter ikisha pata moto kaanga vitunguu (visiwe vya brown) kisha tia tangawizi, swaum, chumvi na spice zote. Kaanga kidogo kisha tia unga wa ngano uchanganye vizuri kisha tia maziwa na uache uchemke kidogo uku ukiwa unakoroga(hakikisha unapata uji mzito kiasi kisha ipua na uwadumbukize samaki humo. Baada ya hapo chukua sufuria ya kuokea na utie viazi na hiyo rojo ya samaki, changanya vizuri kisha mwagia cheese kwa juu na ubake kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo chakula chako kitakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kupika Sambusa Za vegetable

Chef Mishamo

Jinsi ya kupika Sambusa za vegetable

Mahitaji

Viazi 6 vya wastani
Hoho jekundu 1/2
Hoho la kijani 1/2
Vitunguu maji 2 vikubwa
Njegere 1/2 kikombe
Carrots 2 zilizo kwanguliwa
Garlic/ ginger paste 1 kijiko cha chai
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Corinder powder 1/4 kijiko cha chai
Turmaric 1/4 kijiko cha chai
Chilli powder kiasi
Limao 1/2
Chopped coriander kiasi
Chumvi
Manda
Mafuta ya kukaangia

Matayarisho

Menya viazi kisha vichemshe na chumvi kidogo. Vikiiva vimash na uma mpaka vilainike kiasi kisha viweke pembeni. Baada ya hapo katika sufuria isiyoshika tia mafuta kidogo sana. Yakipata moto tia vitunguu maji kaanga kwa muda wa dk 2 kisha ginger/garlic paste kaanga kidogo kisha tia spice zote. Zichanganye vizuri. Baada ya hapo tia vegetable zote zilizobaki pamoja na chumvi, limao zipike pamoja kwa muda wa dk 5.Malizia kwa kutia mashed potato na vimaji kidogo sana. Zichanganye vizuri mpaka vitu vyote vichanganyike kisha ipua. Acha vipoe kisha tia coriander.Baada ya hapo funga kama unavyokunja sambusa za kawaida kisha zichome ktk mafuta.Zikisha iva zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Note:

Inapendeza zaidi vegetable zote (kasoro carrot) kukatwa ktk shape ya cubes ndogondogo.

Mapishi ya Shami Kebab

Chef Mishamo

Mapishi ya Shami kebab

Mahitaji

Nyama ya ng'ombe (steak)1/4 kilo
Dengu kavu 1/2 kikombe
Giligilani ya unga 1/2 kijiko cha chai
Binzari nyembamba ya unga 1/4 kijiko cha chai
Swaum/tangawizi kijiko 1 kikubwa cha chakula
Chumvi kiasi
Curry powder 1 kijiko cha chai
Pilipili kali 1/2
Yai 1
Mafuta ya kukaangia
Kitunguu maji kilichokatwakatwa
Limao 1/2

Matayarisho

Chemsha nyama na limao na chumvi mpaka iwe laini. Na pia chemsha dengu nazo mpaka ziwe laini. Baada ya hapo tia nyama,dengu na spice zote ktk blender (kasoro vitunguu,majani ya giligilani, yai) Visage mpaka viwe laini kisha tia ktk bakuli. Baada ya hapo malizia kwa kutia vitu vilivyobaki.Changanya vizuri kisha tengeneza kebab zako shape ya round (kama uonavyo kwenye picha) kisha zikaange ktk mafuta ya kiasi. Baada ya hapo zitakapoiva zitakuwa tayari kwa kuliwa.Unaweza kuzisev na salad uipendayo

Tomato Concasee/Mother sauce

Ingredients

oil
salt
paper
Bazily
Tomato paste
Tomato Peeled

°Procedures°
Unaandaa Vitu vyako kisha unasotea kwenye Burner

Hivyo tu itakuwa tayari Hii inatumika kutengeneza sauce nyingine ndio maana Inaitwa Mother sauce



powered by
Mishamo Tz
Sir phabian Juma

Mapishi Ya Ndizi Za Nazi Na utumbo

Chef Mishamo


Mapishi ya Ndizi za nazi na utumbo

Mahitaji

Ndizi mshale 10
Utumbo wa ng'ombe 1/2 kilo
Nazi ya kopo 1
Nyanya 1
Kitunguu kikubwa 1
Tangawizi/ swaum 1 kijiko cha chakula
Olive oil kiasi
Limao 1
Chumvi
Curry powder 1 kijiko cha chai
Turmaric 1/2 kijiko cha chai
Coriander ya powder 1/2 kijiko cha chai
Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai
Pilipili kali nzima (usiipasue)

Matayarisho

Safisha utumbo kisha uweke ktk pressure cooker pamoja na chumvi kiasi, limao, tangawizi, swaum na maji kiasi kisha uchemshe kwa muda wa nusu saa. Baada ya hapo menya ndizi kisha zikate vipande vidogo kiasi ili ziwahi kuiva, kisha ktk sufuria ya kupikia tia vitunguu na nyanya kisha ndizi kwa juu yake na supu ya utumbo kiasi chumvi kidogo na mafuta kiasi kisha bandika jikoni na uchemshe mpaka ndizi zikaribie kuiva. Zikisha karibia kuiva tia utumbo na spice zote, pilipili nzima na tui la nazi kisha changanya vizuri na uache vichemke mpaka ndizi na tui la nazi vitakapoiva na rojo ibaki kiasi. Baada ya hapo Ndizi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mkate wa mayai


Chef Mishamo

Mkate wa mayai

Mahitaji

Slice za mkate 6
Mayai 3
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Vunja mayai yote katika sahani kisha tia chumvi kidogo sana na uyapige mpaka chumvi ichanganyike. Kisha chukua frying pan na utie vimafuta kidogo na uweke jikoni. Mafuta yakishapata moto kiasi,chovya slice za mkate katika hayo mayai na uzipike pande zote zikishaiva zitoe na uziweke katika kitchen towel ili kukausha mafuta.Na baada ya hapo mikate yako itakuwa tayari kwa kuliwa na chai.

MAPISHI YA MCHUZI WA KAMBALE

Mapishi ya Mchuzi wa kambale

Mahitaji

Kambale 2
Nazi kopo 1
Nyanya kopo 1
Vitunguu 2
Curry powder 1 kijiko cha chai
Turmaric 1/2 kijiko cha chai
Binzari nyembamba ya unga 1/2 kijiko cha chai
Swaum/ tangawizi 1 kijiko cha chakula
Giligilani kiasi
Limao 1/2
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Loweka samaki katika maji ya moto kwa muda wa muda wa nusu saa.Baada ya hapo Saga pamoja nyanya, vitunguu, swaum na tangawizi kisha vibandike jikoni na uvipike mpaka maji yote yakauke kisha tia mafuta. Pika mpaka nyanya zitengane na mafuta kisha tia spice zote.Zipike kwa muda mdogo kisha tia tui la nazi, maji kiasi, samaki, pilipili nzima, chumvi na kamulia limao. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na samaki pia wawe wameiva na mchuzi ubakie kiasi. Baada ya hapo ipua kisha tia giligilani iliyokatwa na mchuzi utakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuulia kwa chochote kile upendacho. Mi hupendaga kuulia na ugali mlaiiini au na wali pia.

Jumamosi, 7 Oktoba 2017

Mapishi Ya Ndizi Tamu Za Kuoka

Mahitaji

Ndizi tamu 4
Chumvi kidogo
Mafuta

Matayarisho

Menya ndizi kisha zikwangue utomvu. Baada ya hapo zioshe na uzikaushe maji yote na kitchen towel. Baada ya hapo zipasue kati na ukate tena nusu yake.Zipake mafuta pande zote kisha zinyunyuzie chumvi kidogo pande zote. Baada ya hapo zibake kwa moto wa juu na chini mpaka zitakapoiva na kupata rangi ya brown juu na chini. baada ya hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa

Mapishi ya Mihogo ya Nazi Na Kuku

Mahitaji

Mihogo kilo 1
Kidali cha kuku 1 kikubwa
Nyanya 1 kubwa
Kitunguu maji 1 cha wastani
Swaum/tangawizi i kijiko cha chai
Nazi kopo 1
curry powder 1 kijiko cha chai
Binzari manjano 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Pilipili 1
Chumvi kiasi

Matayarisho

Saga pamoja nyanya, kitunguu na swaum/ginger pamoja na vimaji kidogo. Kisha vitie kwenye sufuria isiyoshika chini na uvishemshe mpaka maji yote yakauke kisha tia mafuta na upike ktk moto mdogo mpaka viive.Baada ya hapo tia spice na uzipike kidogo kisha tia mihogo na kuku (kuku na mihogo vikatwe vipande vya wastani) vichanganye vizuri kisha tia nazi  na vimaji kiasi,limao chumvi na pilipili na ufunike kisha punguza moto. Pika mpaka mihogo na kuku viive na ibaki rojo kidogo kisha ipua na mihogo yako itakuwa tayari kwa kuliwa

Mishkaki Ya Kuku

Mahitaji

Kidali cha kuku 1 kikubwa
Swaum,tangawizi 1 kijiko cha chai
Limao 1/2
Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai
Curry powder 1/2 kijiko
Paprika 1/2 kijiko cha chai
Hoho jekundu 1/2
Hoho la njano 1/2
Kitunguu 1/2
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Katakata kuku ktk vipande vya mishkaki ya kawaida kisha vimarinate na vitu vyote, kasoro hoho na kitunguu.Ni vizuri kuziacha either usiku mzima au kwa masaa machache ili spice ziingie vizuri. Baada ya hapo katakata hoho na vitunguu vipande vya wastani kiasi. Baada ya hapo Taarisha vijiti vya mishkaki kisha tunga nyama pamoja na hoho na vitunguu kisha nyunyuzia mafuta na kisha uzichome kama mishkaki ya kawaida. Itakapoiva itakuwa tayari kwa kuliwa na chochote upendacho kama ndizi za kuchoma, viazi na n.k.


Mishamo Tz

Jinsi ya Kutengeneza Tomato Sauce

Jinsi ya kutengenza Tomato Sauc

Mara kadhaa nimekuwa nikileta Makala mbalimbali ambazo zinakupa hamasa tu ila Makala ya leo ni pesa mkononi. Pesa mkononi ndiyo ambayo kila mtu anahitaji. Pia nimeamua kukuletea makala haya ili tuendane sawa na Tanzania ya viwanda.

Najua inawezekana kabisa kila mtu kuwa na kiwanda, unashangaa wala usishangae maana huo ndio ukweli maana kila kitu kinapatikana kiurahisi katika mazingira yetu.

Unajua kuwa mikono yako ndiyo itakayokupa pesa? Kama hufahamu basi nimekuja kukujuza ni kivipi utatumia mikono yako ili uweze kuwa tajiri.

Yafuatayo ndiyo mahitaji ya kutengeneza tomato source.
Nyanya kilo 1.
Vitunguu maji viwili.
Vinegar vijiko 3 vya chai.
Sukari vijiko 2 vya chai.
Chumvi kijiko kimoja cha chai
Maji ya moto kikombe kimoja cha chai.
Mafuta ya kula vijiko 7 ya vyakula.

Haya ndiyo mahitaji ya kutaka kutengeneza tomato souce, hata hivyo kama unataka kutengeneza zaidi ya hapo unatakiwa kuongeza uwiano wa mahitaji hayo.

JINSI YA KUTENGENEZA TOMATO SOURCE.

HATUA YA KWANZA.
A) Menya nyanya na vitunguu kisha vikate vipande vidogo vidogo.
B) Tumia Brenda kusaga mchanganyiko wako.
C) Anza kuweka malighafi namba 1 hadi namba 4 katika brenda yako kutokana na ratio (uwiano ) uliopewa hapo juu. Saga kwa dakika kadhaa hadi uone imetokea rojo laini.

HATUA YA PILI.
A) Tumia sufuria yenye nafasi kupika mseto huu.
B) Weka sufuria yako jikoni tia mafuta ya kula acha yachemke kisha mwagia mseto wako na kisha uanze kukoroga kwa dakika 30 kuelekea upande mmoja huku ukichemka.
C) Baada ya hapo epua mseto huo utakuwa tayari imeshakuwa tomato funga vizuri na kisha peleka sokoni.

Mpaka kufikia hapo wewe Tajiri, na mafanikio makubwa ambayo yatakuwa upande wako endapo utakuwa umeamua kuondokana na umaskini kwa njia ya kutengeneza vitu mbalimbali kwa ajili ya kuuza.

Nikusihi uendelee kufuatana nami katika Makala zijazo ili tuweze kufika mahali ambapo tunatamani kufika.? Endelea kufuatana nasi hapa dira ya mafanikio kwa masomo mengine yanayokuja.





Mishamo Tz

Simple Desserts

Mahitaji

Matunda mchanganyiko (mix fruit) kama vile
Ndizi
Zabibu
Pears (liliova laini)
Nanasi
Strawberry
Embe
Yogurt kiasi
Asali
Cinnamon powder kidogo sana (1/4 ya kijiko cha chai)

Matayarisho

Safisha matunda yote kisha yakaushe maji baada ya hapo yakate katika vipande vidogo vigogo kisha yatie kwenye bakuli safi.Baada ya hapo tia cinnamon na yogurt vichanganye vizuri kisha sawazisha. Malizia kwa kumwagia asali juu yake (kama uonavyo kwenye picha) Unaiweza kuila baada ya hapo au ukaiweka frijini ipate baridi na ikaliwa baadaye.
Dessert hii ni rahisi kutengeneza pia ni nzuri kwa afya ya mlaji kwa sababu haina sukari pia ina matunda. Kwa hiyo ni vizuri zaidi wakati mwingine una avoid ice cream kwa dessert na kutumia hii.

Mapishi Ya Biliganya

Mahitaji

Bilinganya 2 za wastani
Nyanya kubwa 1
Kitunguu maji 1 kikubwa
Swaum 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/4
Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai
Parpika 1/4 kijiko cha chai
Pilipili mtama 1/4 kijiko cha chai
Curry powder1/4 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Coriander
Olive oil

Matayarisho

Katakata bilinganya slice nyembamba kisha ziweke pembeni. Baada ya hapo kaanga kitunguu maji mpaka kiwe cha brown kisha tia swaum na spice zote, zikaange kidogo kisha tia nyanya na chumvi kiasi. Pika nyanya mpaka iive na itengane na mafuta. Baada ya hapo tia mabilinganya na ukamulie limao kisha punguza moto na uyafunike na mfuniko usioruhusu kutoa mvuke ili yaivie na huo mvuke. Baada ya hapo yaonje kama yameiva na malizia kwa kutia fresh coriander na baada ya hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa. kwa kawaida mi hupendaga kuyalia na wali na maharage badala ya kachumari kwahiyo nakuwa naitumia hiyo kama kachumbari






Mishamo Tz

Mapishi ya Supu ya Makongoro

Mahitaji

Makongoro (miguu ya ng'ombe) kiasi
Limao 1 kubwa
Kitunguu swaum
Tangawizi
Chumvi
Pilipili

Matayarisho

Safisha makongoro kisha yatie kwenye pressure cooker. Kisha tia kitunguu swaum, tangawizi, chumvi,limao na maji kiasi. Baada ya hapo yachemshe mpake yaive na yawe malaini na pia ubakize supu kiasi inaweza kuchukua kama dk 45 au saa 1 hivi. Baada ya hapo yaipue na upakue supu yako kwenye bakuli katia pilipili kiasi kisha itakuwa tayari kwa kuliwa.

Note:
Ukiwa unanunua makongoro hakikisha unachukuwa yale yasiyokuwa na manyoya na pia
hakikisha usiyachemshe kupitiliza kwani yakiwa malaini sana utashindwa kuyaenjoy.

Mishamo Tz

Mapishi Ya Viazi Vya Nyama

Mahitaji

Viazi (potato) 1 kilo
Nyama ya ng'ombe 1/2 kilo
Nyanya ya kopo iliyosagwa 1/2 tin
Vitunguu maji 2
Tangawizi/ swaum 1 kijiko cha chai
Hoho 1
Curry powder 1 kijiko cha chai
Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Chumvi
Coriander
Mafuta ya kupikia

Matayarisho

Safisha na katakata nyama ktk vipande vidogovidogo kisha weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia nyama, swaum/ tangawizi, chumvi na limao. Ichanganye vizuri kisha funika na uipike mpaka iive na maji yote yakauke yani yabaki mafuta tu. Baada ya hapo tia viazi vilivyokatwa vipande vya wastani vikaange kwa muda wa dakika 10 kisha tia pilipili na curry powder na nyanya. Funika na punguza moto.Pika mpaka nyanya iive vigeuze kisha tia vimaji kidogo vya kuivishia viazi. Viazi vikikaribia kuiva(hakikisha vinabaki na rojo kidogo) tia hoho na upike kwa muda wa dk 5 kisha malizia kwa kutia coriander. Changanya vizuri kisha ipua na viazi vyako vitakuwa tayari kwa kuliwa.




Mishamo Tz

Salad( _Kachumbari)

Mahitaji

Tango 1/2
Kitunguu 1/2
Cherry tomato 8
Lettice kiasi
Green olives kidogo
Black olives kidogo
Hoho jekundu 1
Carrot
Giligilani kidogo
Salad dressing
Yogurt 1/2 kikombe
Swaum 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Pilipili ya unga 1/4 kijiko cha chai
Chumvi kidogo
Olive oil kiasi

Matayarisho

Osha vitu vyote kisha vikaushe maji. Baada ya hapo ktk bakuli kubwa katakata, lettice, tango,hoho, kitunguu,giligilani na kisha ikwangue carrot na utie bila kusahau nyanya zote pamoja na olives.Baada ya hapo ichanganye vizuri, kisha tengeneza salad dressing kwa kuchanganya vitu vyote vilivyo (kwenye list ya salad dressing) kisha koroga vizuri.Baada ya hapo ichanganye na salad.Na hapo salad yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila na chochote upendacho kama vile chips, nyama choma au au chakula kikuu.

Mapishi Ya Maharage Na Spinach

Mahitaji

Maharage yaliyochemshwa kiasi
Spinach zilizokatwa kiasi
Vitunguu maji 2
Nyanya 1/2 kopo
Swaum/Tangawizi 1 kijiko cha chakula
Curry powder 1 kijiko cha chai
Olive oil
Chumvi

Matayarisho

Kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia tangawizi/swaum kisha nyanya. Pika mpaka nyanya ziive kisha tia curry powder na chumvi. Vipike kiasi kisha tia maharage na maji kidogo kisha funika na uache vichemke. Baada ya muda tia spinach vipike pamoja na maharage mpaka ziive kisha ziipue. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuseviwa.








Chef
Mishamo Tz

Caramel Custard

Mahitaji

Mayai 4
Maziwa kikombe 1
Vanilla 1/2 kijiko cha chai
Sukari 1/2 kikombe cha chai

Matayarisho

Changanya pamoja mayai, maziwa, vanilla na robo ya sukari kisha visage katika blender (kama huna blender unaweza kutumia egg whisk) mpaka vichanganyike vizuri kisha chuja mchanganyiko wako na uweke pembeni. Baada ya hapo chukua sukari iliyobaki na utie vimaji kidogo kisha uipike mpaka ibadilike rangi na kuwa light brown kiasi kisha isambaze vizuri katika hiyo sufuria. Baada ya hapo tia mchanganyiko wako katika hiyo sufuria yenye sukari iliyoyeyushwa, kisha chukua tray ya kubake tia maji kiasi na uiweke sufuria iliyokuwa na mchanganyiko wako juu yake, Ibake kwa moto wa chini mpaka itakapokuwa ngumu inaweza kuchua kama dakika 45 au saa 1. Baada ya hapo chukua sahani pana funika juu yake kisha ipindue sufuria ili kuitoa katika sufuria. Baada ya hapo iache ipoe na hapo itakuwa tayari kwa kuliwa