Mishamo Tz

Alhamisi, 13 Septemba 2018

Nyama ya kukaanga

Nyama ya kukaanga

Chef Mishamo TZ

Kuandaadakika 15 
Mapishidakika 30

Walaji: 3

Ujuzi: Rahisi

Nyama rahisi kuandaa na tamu kula. Ni nyama inayokaangwa bila mafuta ya kula na inaweza kuliwa ndani ya dakika 20. Kwenye mboga hii unaweza kuongeza viungo unavyopendelea ili kupata mboga bora na tamu. Ni nyama nzuri ya kula kwa ugali na hata wali.

Mahitaji

Nyama ½ Kilo
Tangawizi ya unga kijiko 1
Mafuta ya kula, nimetumia mafuta ya zaituni (Olive)
Kitunguu maji 1,
kata vipandeLimao 1
Kitunguu saumu punje 5,
pondaPilipili hoho 2, mie nimechanganya za rangi tofauti

Chumvi kijiko 1
Pilipili manga ya unga kijiko 1
Pilipili 2  (cayenne pepper)

Maelekezo

Ni nyama nzuri ya kula kwa ugali na hata wali.

Andaa nyama kwa kuikata vipande vipande na vyembamba ili viive vizuri na kwa urahisi. Osha na kisha weka pembeni ipate kukauka.Paka chumvi pande zote za nyama. Nyunyizia limao, tangawizi, kitunguu saumu kilichopondwa. Paka vizuri pande zote hadi zienee. Weka pilipili manga, paka vizuri. Acha nyama ikae pembeni iingie viungo kwa dakika 10 hadi 15.Bandika kikaango jikoni, acha kipate moto kiasi. Weka nyama, zipange ili zisipandiane. Usiweke mafuta. Acha nyama ziive taratibu huku ukiwa unageuza taratibu. Geuza hadi nyama iwe rangi ya kahawia pande zote na kusiwe na damu wala maji. Hakikisha haiungui. Kama nyama haijaiva na inakauka, nyunyizia maji kiasi ili ipate kulainika vizuri na kuiva kabla ya kuila.

Kuchanganya na mboga mboga

Osha kisha kata pilipili hoho, kitunguu saumu, kitunguu maji na pilipili za kawaida. Hifadhi kwenye chombo safi pembeni.Nyama ikishaiva vizuri, weka mafuta ya kula vijiko 2, acha yapate moto kiasi kisha weka kitunguu maji, koroga vizuri. Funika kiasi ili vitunguu vipate kulainika na kuiva vizuri na kuwa rangi ya kahawia.Weka mboga mboga zilizobaki, kwa awamu. Koroga kila wakati kisha funika na mfuniko. Acha mboga iive kwa mvuke kwa dakika 5 hadi 7. Hakikisha haiungui.Bandua mboga, tenga pembeni na uandae chakula cha kujiramba nacho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni