Mishamo Tz

Jumatatu, 29 Oktoba 2018

MAPISHI YA CHICKEN SATAY

Mapishi ya Chicken Satay

Chef 
Mishamo

Mahitaji

Kidali cha kuku 1 (chicken breast)

Kitunguu maji 1/2 (onion)

Kitunguu swaum/tangawizi (garlic and ginger

paste) 1 kijiko cha chai

Limao ( lemon)1/4 kijiko cha chai

Curry powder 1/4 kijiko cha chai

Pilipili ya unga kidogo (Chilli powder)

Coriander powder 1/4 kijiko cha chai

Soy sauce 1kijiko cha chai

Mafuta 2 vijiko vya chai.

Chumvi kiasi (salt)

Vijiti vya mishkaki

Matayarisho

Osha kidali kisha kikaushe maji na kitchen towel na ukate vipande(cubes) vidogodogo na uweke pembeni. Baada ya hapo changanya vitu vyote

(kasoro vijiti )na utie vimaji kidogo kisha visage katika breda kupata paste nzito. Baada ya hapo changanya hiyo paste na kuku na uache

zimarinate kwa muda wa saa moja. Baada ya hapo zitunge kuku katika vijiti vya kuchomea na uzichome katika oven mpaka ziive (inaweza kuchukua kama dakika 10). Baada ya hapo chicke

Jumamosi, 15 Septemba 2018

Kashata za maziwa ya unga

KASHATA ZA MAZIWA YA UNGA

MAHITAJI

Maziwa ya unga kikombe 1 na nusu

Sukari kikombe 1 na robo

Maji kikombe 1 na nusu

Arki ya vanilla kijiko 1 cha kula

Rangi ya chakula kjk 1 cha kul(orange)

Mafuta ya kupikia vjk 2 vya kula

MATAYARISHO

Kwenye sufuria au pan tia maji na sukari , wacha ichemke
Ikianza kutoa mapovu mazito ( dakika 8 hadi 10) tia rangi , arki na mafuta ya kupikia , koroga kg wacha ichemke tenaSubiria tena kwa dakika 3 mpaka 5 au iwe nzito ukiigusa kwa vidole viwili ukiwachia ifanye kama uzi au mfano wa gundi

Tia maziwa ya unga koroga haraka haraka kwa dkk 1 au mpaka mchanganyiko uwe mzito

Pakaza mafuta sehem yako ya kukatia au trey , weka mchanganyiko wako, tumia mwiko,kijiko au kifimbo kuwekea sawa,  wacha upoe na ukate shape unayopenda

Faida 10 za kunywa maziwa

Faida 10 za Kunywa Maziwa Usizozifahamu

Maziwa hufanya mambo mengi mazuri kwa ajili ya afya yako. Wataalamu wa afya na wauzaji wa maziwa wamekuwa wakieleza faida kadha wa kadha za kunywa maziwa. Je umewahi kujiuliza hasa ni faida gani hizo zitokanazo na unywaji wa maziwa?

Ni wakati wako sasa wa kujiuliza kwa kina juu ya faida zitokanazo na unywaji wa maziwa. Fuatana nami katika makala hii nikueleze faida 10 zitokanazo na unywaji wa maziwa.

1. Hujenga na kulainisha ngozi

Je unamfahamu Cleopatra? Cleopatra alikuwa ni malikia wa Misri anaesadikiwa kuwa mzuri sana. Inaaminikia uzuri wa Cleopatra ulitokana na tabia yake ya kuogea maziwa mara kwa mara.

Hivyo basi, ni wazi kuwa, vitamini na virutubisho vilivyoko katika maziwa ni muhimu kwa ajili ya ngozi bora. Ni vyema kunywa angalau bilauri moja ya maziwa kila siku.

2. Huimarisha meno

Maziwa ni chanzo bora cha madini ya kalisiamu, hivyo basi maziwa ndicho kitu halisi kinachohitajiwa na meno yetu. Pia maziwa huzuia kutoboka na kuoza kwa meno. Kalisiamu hufyonzwa na miili yetu kukiwa na vitamini D; hivyo jitahidi kunywa maziwa kwani maziwa huwa na vitamini D.

3. Huimarisha mifupa

Ni ukweli usiopingika kuwa watoto wanahitaji kunywa maziwa ili kuimarisha ukuaji wao. Ni kweli pia watu wazima wanahitaji kunywa maziwa ili kulinda na kuimarisha mifupa yao dhidi ya magonjwa kama vile udhaifu wa mifupa (osteoporosis). Maradhi haya huzuiliwa kwa kalisiamu ipatikanayo kwenye maziwa na ambayo hufyonzwa kutokana na uwepo wa vitamini D.

4. Kujenga misuli

Maziwa yana mchango mkubwa katika ukuaji wa misuli. Hili ni kutokana na protini zinazopatikana katika maziwa. Wanariadha wengi hunywa maziwa baada ya mazoezi, hii ni kwa ajili ya kuupa mwili virutubisho vya kutosha kwa ajili ya kujijenga tena. Maziwa huzuia maumivu ya misuli pamoja na kurudisha ute ulipotea kwenye misuli wakati wa kazi mbalimbali.

5. Kupunguza uzito

Utafiti unaonesha kuwa wanawake wanaokunywa maziwa hupunguza uzito zaidi kuliko wale wasiokunywa. Inashuriwa kunywa maziwa wakati wa chakula cha jioni au unapokula matunda. Pia maziwa yanaweza kutumiwa kama kileta hamu ya kula yaani appetizer.

6. Huondoa msongo wa mawazo

Hebu fikiri juu ya vitamini na virutubisho vilivyoko kwenye maziwa; hivi huweza kuondoa msongo. Baada ya kazi nyingi za siku, inashauriwa kunywa angalau bilauri (glass) moja ya maziwa ya uvuguvugu. Hili litakusaidia kukuondolea msongo katika misuli na neva zako za fahamu.

7. Huzuia maumivu wakati wa hedhi

Wanawake wengi wanakabiliwa na maumivu wakati wa hedhi. Maziwa yamedhibitishwa kuzuia na kupunguza maumivu haya kwa kiasi kikubwa.

8. Huongeza nguvu za mwili

Je unaishiwa nguvu mapema au kuchoka sana? Kama jibu ni ndiyo, unahitaji virutubisho vilivyoko kwenye maziwa. Hivi vitaupa mwili wako nguvu mpya na kukufanya kuwa mwenye nguvu na furaha siku nzima.

9. Huondoa kiungulia

Kiungulia huwasumbua sana watu wengi. Kiungulia husababishwa na asidi zipatikanazo tumboni. Hivyo maziwa (ambayo si mgando) hutengeneza utando maalumu tumboni ambao hupambana na asidi hizi.

Kwa hiyo nywaji wa maziwa (ambayo si mgando) utakusaidia kupambana na tatizo la kiungulia ndani ya muda mfupi.

10. Hupambana na maradhi mengine

Kwa miongo kadhaa tafiti zimebaini kuwa maziwa huzuia magongwa kadha wa kadha. Magonjwa hayo ni kama vile shinikizo la damu na kiharusi. Inaaminika pia maziwa hupunguza lehemu (cholesterol) mwilini na kuongeza uwezo wa macho kuona. Baadhi ya watafiti wameeleza kuwa unywaji wa maziwa huzuia ania fulani za saratani.

Hitimisho

Yaliyozungumziwa hapa ni faida 10 za kunywa maziwa. Naamini umebaini kuwa maziwa yana manufaa mengi sana kwa ajili ya afya yako zaidi ya haya yaliyotajwa. Ni jambo jema kujizoesha kula vitu vya asili, kwani ndivyo huhitajiwa zaidi na mwili wa mwanadamu. Jizoeze kunywa angalau bilauri moja ya maziwa kila siku kwa ajili ya afya ya mwili wako.

Je una maoni gani kuhusu makala hii? Je wewe huwa unakunywa maziwa? Tuandikie maoni yako hapo chini kisha washirikishe na wengine. Karibu

JUICE YA UBUYU

JE UNAJUA JINSI YA KUTENGENEZA JUISI YA UBUYU???soma hapa.........

© Mishamo TZ

Miaka hii yakaribuni ubuyu umekua tunda lenye jina kubwa sana kwenye jamii yetu ya kitanzania,unasifika kwa kua na virutubisho vingi hasa calcium na Iron

Ubuyu hufaa sana kwa Wajawazito,watoto na wazee,kwani makundi haya yanauhitaji mkubwa wa calcium na iron.
Namna nzuri na rahisi ya kufanya ubuyu sehem ya lishe  ni kwa kuutumia kutengeneza juisi
Juisi ya ubuyu imekua maarufu sana katika jamii yetu na inapendwa sana.Mimi mwenyewe ni mmoja wa wapenzi wakubwa wa juice ya ubuyu.Ingawa unaweza changanya ubuyu na matunda mengine,mimi napenda kunywa juice ya ubuyu pekeyake.Wakati mwingine naiwekea rangi na kuongezea vanila ili tu kuipa sura na harufu ya tofauti.
Watu wengi hawachemshi juisi ya ubuyu,Jambo ambalo ni hatarishi ki afya.Chemsha ubuyu ili kuuwa vijidudu viletavyo magonjwa,ubuyu hupita kwenye mikono ya wengi kabla haujakufikia wewe mtumiaji,na pia hujui ulitunzwa katika mazingira gani.Ni vyema kuchukua taadhari kwa kuchemsha.

© MAHITAJI

Ubuyu(wa unga au wa mbegu)
Maji
Sukari

© NJIA

1.Chambua ubuyu,ondo uchafu wowote uliopo kwenye ubuyu

2.Katika sufuria,weka ubuyu kisha ongeza maji.Katika kila kipimo cha ubuyu ongeza maji mara tatu yake
Ubuyu wa mbegu vikombe 6  weka maji vikombe 9
Ubuyu wa unga  vikombe 3 weka maji vikombe 12

3.Funika sufuria kisha bandika jikoni,chemsha adi vitokote,vipe  angalau dakika nne za kutokotea.
002

Kumbuka maji unayotumia kuchemsha ubuyu ni maji ya bomba na si salama,hivyo ni muhim kuyapa  muda mzuri wa kuchemka ili juice yako iwe salama.

4.Juisiinapoanza tu kutokota ongeza sukari kwa ladha uipendayo kisha acha zile dakika nne za kutokota ziishe.Zima jiko acha juisi ipoe.
Napenda kuweka sukari ichemkie kwenye juice kwani inafanya juice ishikane na kua nzito.Sukari ikichemshwa inakawaida ya kua nzito.Kumbuka kwamba ubuyu ni mwepesi sana na juice yake kawaida hujitenga inapotulia,ubuyu waenda chini na maji yanabaki juu.Ukichemsha sukari inasaidia kuondoa hali hiyo.

5.Chuja juisi,ongeza maji kama unaona ni nzito sana,na ongeza sukari endapo ile uliyoweka awali haitoshi.Juisi tayari kwa kunywa.

Maelezo ya ziada.

Kama unampa mtoto mdogo juice hii,basi acha itulie ili unga au chembechembe za ubuyu ziende chini,kisha chukua juisi nyepesi iliyobaki juu nsio umpe mtoto.Juice ya ubuyu nzuri sana kwa mtoto kwani ina calcium kwa wingi.

Alhamisi, 13 Septemba 2018

Nyama ya kukaanga

Nyama ya kukaanga

Chef Mishamo TZ

Kuandaadakika 15 
Mapishidakika 30

Walaji: 3

Ujuzi: Rahisi

Nyama rahisi kuandaa na tamu kula. Ni nyama inayokaangwa bila mafuta ya kula na inaweza kuliwa ndani ya dakika 20. Kwenye mboga hii unaweza kuongeza viungo unavyopendelea ili kupata mboga bora na tamu. Ni nyama nzuri ya kula kwa ugali na hata wali.

Mahitaji

Nyama ½ Kilo
Tangawizi ya unga kijiko 1
Mafuta ya kula, nimetumia mafuta ya zaituni (Olive)
Kitunguu maji 1,
kata vipandeLimao 1
Kitunguu saumu punje 5,
pondaPilipili hoho 2, mie nimechanganya za rangi tofauti

Chumvi kijiko 1
Pilipili manga ya unga kijiko 1
Pilipili 2  (cayenne pepper)

Maelekezo

Ni nyama nzuri ya kula kwa ugali na hata wali.

Andaa nyama kwa kuikata vipande vipande na vyembamba ili viive vizuri na kwa urahisi. Osha na kisha weka pembeni ipate kukauka.Paka chumvi pande zote za nyama. Nyunyizia limao, tangawizi, kitunguu saumu kilichopondwa. Paka vizuri pande zote hadi zienee. Weka pilipili manga, paka vizuri. Acha nyama ikae pembeni iingie viungo kwa dakika 10 hadi 15.Bandika kikaango jikoni, acha kipate moto kiasi. Weka nyama, zipange ili zisipandiane. Usiweke mafuta. Acha nyama ziive taratibu huku ukiwa unageuza taratibu. Geuza hadi nyama iwe rangi ya kahawia pande zote na kusiwe na damu wala maji. Hakikisha haiungui. Kama nyama haijaiva na inakauka, nyunyizia maji kiasi ili ipate kulainika vizuri na kuiva kabla ya kuila.

Kuchanganya na mboga mboga

Osha kisha kata pilipili hoho, kitunguu saumu, kitunguu maji na pilipili za kawaida. Hifadhi kwenye chombo safi pembeni.Nyama ikishaiva vizuri, weka mafuta ya kula vijiko 2, acha yapate moto kiasi kisha weka kitunguu maji, koroga vizuri. Funika kiasi ili vitunguu vipate kulainika na kuiva vizuri na kuwa rangi ya kahawia.Weka mboga mboga zilizobaki, kwa awamu. Koroga kila wakati kisha funika na mfuniko. Acha mboga iive kwa mvuke kwa dakika 5 hadi 7. Hakikisha haiungui.Bandua mboga, tenga pembeni na uandae chakula cha kujiramba nacho.

Jumapili, 2 Septemba 2018

NJEGELE ZA NAZI

Njegere za Nazi

Posted by mishamo Chef in Mboga
habari za muda wapenzi wa blogu yetu ya Mapishi. leo tutapika njegere za nazi, njegere zinaweza kupikwa kwa namna tofauti tofauti, unaweza kuzitia kwenye wali, pilau, unaweza kuzipika na nyama na hata kwenye tambi hupendeza. leo njegere zetu sie tutaziunga kwa kutumia nazi.

Pishi: Njegere za Nazi
Mahitaji

1.njegere nusu kilo
2.nazi 2
3.nyanya 4
4.Karoti 1
5.Pilipili hoho 1
6.Kitunguu maji 1
7.Thoum kiasi
8 . mafuta ya kupikia kiasi
9.Chumvi kiasi
Jinsi ya kupika njegere za nazi hatua kwa hatua
njegere hizi zinapendeza kuliwa na wali, ukipata kachumbari na juisi pembeni bila kusahau nyama za kukaanga hunoga zaidi. karibuni

chambua njegere, zikoshe, kisha zitie kwenye sufuria na maji uzichemshe ziive kiasi lakini zisilainike sana. 1
safisha nyanya uzimenye na kuzikata. Pia katakata hoho, karoti na vitunguu. Twanga vitunguu thoum. kisha kuna nazi uchuje tui zito na jepesi. 2
bandika sufuria jikoni, weka mafuta ukaange vitunguu, vikishabadilika rangi tia hoho kaanga kidogo kisha utie thoum na nyanya pamoja na karoti, endelea kukaanga. 3
mimina njegere, tia chumvi na umimine tui jepesi, wacha lichemke. kisha tia tui zito liache lichemke kiasi na uzito wa njegere ukiwa sawa, tayari epua.

JINSI YA KUANDAA KUKU WA KUJAZA

Jinsi ya Kuandaa Kuku wa Kujaza

Posted by mishamo Chef

Kuku wa Kujaza: Kuku ni moja kati ya kitoweo kipendwacho na wengi, kuku kitoweo, vitumbua, mboga, mchuzi, supu, yote mapishi yake. Leo tunaandaa kuku wa kujaza ambaye kwa jina jengine huitwa kuku wa mahshai. Tunamuandaa mzima bila kumkatakata, tunatoa vitu vyake vya ndani, tunamtengeneza na kisha tunamjaza wali, ni zuri hili pishi hivyo nakusihi usiende mbali na jiko letu.

Mahitaji

Kuku mkubwa 1
mafuta lita 1
mchele nusu kilo
vitunguu nusu kilo
tangawizi kiasi
thoum na uzile kiasi
hiliki na zabibu kidogo
chumvi vijiko 2
Kuandaa Kuku wa Kujaza hatua kwa hatua
Kuku wetu wa kujaza tayari, na sio lazima umjaze wali mweupe, waweza kumjaza wali wa njegere, pilau, wali wa karoti, wali wa manjano na hata chipsi. Natumai tumefaidika na somo la leo namna ya kuandaa kuku wa kujaza, karibuni sana.

Chukua kuku aliyekwisha nyonyolewa vizuri na kutolewa vitu vya ndani, bila kumkata vipande mchemshe kwa maji na chumvi, mtie vitunguu, thoum, tangawizi na uzile ( viungo vyengine vibakishe). Mwache achemke pamoja na hivyo viungo mpaka maji yakauke. 1
Weka mafuta kwenye sufuria jikoni, umkaange kuku wako mpaka awe mwekundu. Kisha muepue muweke pembeni 2
Bandika sufuria, itie mafuka kiasi kiaha kaange vitunguu kidogo, kisha tia thoum na viungo vyote vilivyobakia ukaange 3
Chemsha mchele utie na chumvi, uuache uive kiasi. Kisha uchuje maji yote. Uchukue uutie kwenye ile sufuria yenye viungo tuliovikaanga ukoroge pamoja hadi ukauke. Fukua kidogo kati utie zabibu kavu, kisha uupalie kama wali wa kawaida 4

ukishakuwa tayari wali, upakue uutie kwenye tumbo la kuku kisha umshikize kwa uzi mwembamba ili wali usitoke, hapo mueke kwenye sahani umpambe uwezavyo kwa saladi na mbogamboga. Kuku wetu tayari.

JINSI YA KUPIKA CHICKEN WITH MASHED POTATOE

Mahitaji

Kuku aliyetolewa ngozi tayari robo kiloButter vijiko 2Pilipili manga kijiko 1 chaiNyanya 2Nyanya ya kopo kijiko 1Tangawizi iliyosagwa kijiko 1Viazi ulaya robo kiloChumvi kijiko kimoja cha chaiKitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1Kitunguu maji 1karoti 1Pilipili hoho 1Gram masala kijiko 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Chemsha kuku, weka tangawizi, kitunguu saumu, mkamulie ndimu na chumvi. Hakikisha ameiva na supu imebaki kidogo.Toa nyama iweke kwenye chombo pembeni, tayari kwa kuliwa.Chukua sufuria, weka butter kijiko kimoja ikipata moto weka kitunguu maji, kitunguu saumu, pilipilipili hoho na karoti, koroga mboga ziive ila zisiive sana.Weka nyanya ikichemka, weka nyanya ya kopo na gram masala koroga mpaka uhakikishe nyanya vimeiva kisha ongeza maji kidogo, funika sauce ichemke kisha epua weka pembeni.Menya viazi, kata saizi unayotaka, weka supu ya kuku kidogo, hakikisha viazi vinaiva na havipondeki.Vikiiva epua, weka viazi kwenye bakuli au sufuria, weka pilipili manga, butter yenye chumvi na maziwa kwenye viazi.Anza kuponda viazi, viponde kwa mwiko au visage kwenye blender hakikisha visiwe uji, viwe kama ugali.Ukiona tayari weka pembeni.Chukua sahani pakua viazi, weka sauce na kipande cha kuku, hapo utakua tayari kujiramba.

JINSI YA KUTENGENEZA JUICE YA PARACHICHI NA MAZIWA

MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Parachichi kubwa kiasi 1
 1 Medium Size Avocado

2.Maziwa Ya Unga Kikombe kidogo cha chai Nusu 
 1/2 Cup Milk Powder

3.Sukari Vijiko Vikubwa 5
 5 Tbsp Sugar

4.Arki ya Ice Cream Kiduchu
 Ice Cream Essence to taste

5.Maji ya Baridi Lita Moja na Nusu
 1.5 Litre Cold Water

6.Ndizi mbivu 1
 1 Ripen Banana

7.Ndimu Kipande 
 Small Piece Lemon

MAANDALIZI/PREPARATION
1.Osha Parachichi kwa maji safi Vizuri
  Rinse Avocado well with clean water 

2.Kisha limenye na toa kokwa(Tunda) la katikati ya parachichi 
  Peel it and remove the inner seed of avocado 

3.Kata vipande vidogo vidogo weka kwenye jagi la blenda
 Cut the avocado into small pieces and put them into blender jug

4.Menya Ndizi na katakata weka kwenye blenda
 Peel the banana and cut into pieces then add into jug too

JINSI YA KUANDAA/HOW TO PREPARE
1.Weka maziwa,sukari na maji kwenye jagi la blenda uliloweka parachichi na ndizi
 Add the milk,sugar and water in the jug has the mixture of avocado and banana

2.Saga mchanganyiko wako kiasi cha dakika 3
 Blend the mixture for at least 3 minutes

3.Weka arki na endelea kusaga kwa dakika 3 
 Add the Ice cream essence and keep blending the mixture

4.Malizia kwa kukamua ndimu na weka maji yake kisha saga kwa dakika 2 tu
 Finally squeze the lemon and add lemon juice in the mixture for 2 minutes

5.Mimina kwenye chupa weka katika friji ipate baridi kiasi usiache mpaka ikafanya barafu
  Pour in the jug or bottle refrigerate but make sure it does not freeze

6.Ikiwa na baridi nzuri unaweza kunywa na mkate au vileja ,keki n.k
 After getting cold you may serve with bread,cake etc

Angalizo:Note
1.Parachichi lazima liwe gumu kidogo lisiwe laini sana
  Don’t use rippen Avocado

2.Hakikisha haiwi nzito sana wala nyepesi sana itapoteza ladha yake 
 The juice consistence should neither be lighter nor heavier

3.Sio lazima kuweka ndimu
 Lemon juice is optional

4.Usiweke kwenye friza ikiganda itapoteza utamu
  Dont freeze the juice just refrigerate it

5.Usiongeze tunda jengine lolote 
 Dont add any other fruit may change the taste

JINSI YA KUTENGENEZA SMOOTHIE YA PAPAI NA NDIZI

Jinsi ya kutengeneza smoothie ya papai na ndizi VIPIMO:

🔸Papai dogo 1, lilomenywa na kukatwa katwa
🔸Ndizi mbivu 2 ,zilizomenywa na kukatwa katwa
🔸Maziwa vikombe 2 1/2 au kiasi yanahitajika
🔸Vanilla kijiko 1 cha chai

NAMNA YA KUTAYARISHA:-

1. Tia mahitaji katika blender kisha saga hadi mchanganyiko uwe laini. Enjoy!

✴Smoothie hii itakusaidia mmeng’enyo wa chakula, kutoa gas tumboni na kukupa nguvu..Ni nzuri sana kufungulia kinywa.

JINSI YA KIPIKA TAMBI ZA MAYAI

Jinsi Ya Kupika Tambi Za Mayai.

Najua kila wakati tumekuwa tukikuletea makala mbalimbali ambazo kimsingi zimekuwa zikikusaidia kwa namna moja ama nyingine katika kuulisha ubongo chakula ya akili. Au kwa maneno mengine elimu ambayo umekuwa ukiipata hapa imekuwa ikikusaidia kuzaliwa upya kifikra hatimaye kutimiza kusudio lako hapa duniani.

Lakini katika makala ya leo nataka tujikite katika masuala mazima ya mapishi. Najua utakuwa unashangaa vipi leo afisa mipango kuleta somo hili. Wala usishangae kila kitu ambacho unakiona katika dunia hii ni fursa.  Inawezekana kabisa ukawa hauna lengo la kupika aina hii cha chakula. 

Ila kutokana na ulichojifunza hapa kukusaidia kutoa elimu kwa watu wengine na wao wakalipa pesa au chakula hiki unaweza ukakipika katika sehemu mbalimbali kama katika sherehe mbalimbali na wageni waalikwa na wasio waalikwa wakafurahia aina hii cha chakula. 


Au unaweza ukapika aina hii ya chakula kwa ajili ya biashara kama vile kwenye mahoteli, migahawa na sehemu nyinginezo.

Hebu tuangalie mahitaji kwa ajili ya kupika aina hii cha chakula. 

1. Tambi 1/2 paket

2. Vitunguu maji 2 vikubwa

Karoti 1

3. Vitunguu swaumu kijiko 1 cha chakula

4. Carry powder kijiko 1 cha chai

pilipili hoho 1

5. Njegere zilizo chemshwa 1/2 kikombe

6. Mafuta ya kupikia kiasi

7. Chumvi kwa ladha upendayo

MAANDALIZI YA CHAKULA HIKI

a) Chemsha maji yachemke haswaa, tia chumvi na mafuta kiasi, weka tambi katika maji yaliyo chemka ziache ziive kiasi; kisha chuja maji na uziache kavu.

b) Chukua bakuli pasua mayai kisha weka pembeni.

c) Chukua kikaango kilicho safi weka jikoni tia mafuta kiasi na utaendelelea kuweka vitunguu maji,vitunguu swaumu,hoho ,karoti na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo mdogo na havitakiwi kuiva sana.

d) Kisha tia tambi na njegere katika mchanganyiko wako na uendelee kukaanga kwa dakika kadhaa.

e) Chukua mayai tia katika tambi ongeza moto kiasi, ili tambi zako zichambuke ,moto hautakiwi kuwa mdogo sana ikiwa moto ni mdogo tambi zako zitashikana na kutia mabonge , mayai ya kiiva hapo chakula chako kitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mpaka kufikia hapa chakula chako kitakuwa tayari kwa ajili ya kuliwa, chakula hiki wakati wa kula unaweza ukawa unashushia na juisi ambayo unayopendelea kunywa. 

"Mwili hujengwi kwa mawe bali hujengwa kwa kula"