Mishamo Tz

Jumatano, 19 Oktoba 2022

WALI WA PILAU

​WALI WA PILAU

viambata


Mchele kilo 1


Nyama kilo 1


Samli  kilo


Vitunguu maji  kilo


Vitunguu thomu gram 100


Tangawizi mbichi gram 100


Mdalasini gram 50


Hiliki gram 25


Pilipili manga gram 100


Zabibu gram 100


Chumvi kiasi


1                    Teleka nyama utie chumvi na maji uipike mpaka iive. Baadae epua uiweke (ubakishe supu itakayotosha kuweza kuivisha mchele).


2                    Menya vitunguu uvikate. Menya vitunguu thomu na tangawizi mbichi utwange pamoja. Menya hiliki uitwange pamoja na bizari nzima. osha vijiti vya mdalasini pamoja na chembe za pilipilimanga uziweke. Osha zabibu uziweke. Menya mbatata uzioshe uziweke.


3                    Teleka sufuria tia samli, ikichemka tia vitunguu uvikaange. Tia thomu na tangawizi mbichi uliyoisaga tia vipande vyote vya nyama bila supu, tia mbatata na viungo vyote ulivyovisaga na kuviosha, isipokuwa zabibu. Kaanga kwa muda mfupi, baadae tia supu yote. Ikianza kuchemka tia mchele, onja chumvi. Angalia kiini cha mchele, ukiona wali umeiva na kukauka, fukua kati utie zabibu zote na baadae funika upalie moto.

Jumatano, 21 Septemba 2022

JINSI YA KUPIKA VIAZI VYA NYAMA VYA NAZI

​JINSI YA KUPIKA VIAZI VYA NYAMA VYA NAZI(STYLE 2)


 



Miongoni mwa vyakula vinavyonidondosha mate na kunifanya nile mpaka nivimbiwe ni viazi vya nazi. Ninapoulizwa nyumbani ni chakula gani tupike basi viazi vya nazi havikosekani kwenye orodha. Naam! Viazi vya nazi ni chakula maarufu mno Mombasa na kote pwani Kwa ujumla. Vile vile ni chakula ambacho kwamba ni nadra sana kukosekana wakati wa ramadhani.  Pengine huenda kisipikwe mwaka mzima lakini Ramadhani ni lazima kitapikwa japo siku chache. Hili ni dhihirisho kuwa ni chakula kinachoenziwa na wengi. Bila shaka kama hukifahamu chakula hiki basi una hamu kuu ya kujua kinavyoandiliwa. Ungana nami tujifunze Kwa pamoja! Kumbuka! Raha ya viazi vya nazi ni vikolee nazi.


MAHITAJI


viazi kilo 1 vilivyochambuliwa maganda na kukatwa Kwa slices (hakikisha slices si nyembamba sana ili viazi visivurugike)

Nyama 1/2 kilo iliochemshwa na Chumvi (usiiache na supu nyingi kwasababu kuna matusha)

Tomato 2

Kitunguu maji 1

Pilipili boga/hoho 1

Dania 1

Kitunguu thomu kilichosagwa kijiko 1 cha mezani

Curry powder kijiko 1 cha mezani

Matusha(tui jepesi) vikombe 3

Tui zito kikombe 1

Chumvi kiasi


MATAYARISHO


Weka viazi kwenye sufuria kisha ukatie Katia ndani yake tomato,  Kitunguu maji,pilipili  boga na dania

Weka Kitunguu thomu, currypowder, chumvi na matusha ufunike viazi vyako viendelee kuiva Kwa moto wa kiasi

Kama viazi bado vigumu utaongeza matusha kidogo(hakikisha umeweka matusha ya akiba pembeni)

Viazi vikielekea kuiva weka nyama(kama nyama ni ngumu Sana unaweza ukaiweka mwanzoni wakati ukiweka tomato na vengivyengi)

Viazi vikishaiva, weka tui zito(unaweza ukaweka royco  ukakorogea ukipenda)

Acha itokote Kwa dakika 3 na viazi vipo tayari

Andaa Kwa pilipili ya ndimu