Mishamo Tz

Jumamosi, 30 Septemba 2017

Zitto Kabwe Atoa Neno Juu ya Mauaji ya Polisi kufanya Uchunguzi

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe amelitaka Jeshi la Polisi kufanyia uchunguzi wa kina matukio ya kiuhalifu yanayopelekea kuuawa kwa viongozi kwa madai kitendo hicho kinakaribisha siasa ya damu kuzoeleka katika taifa

Zitto amebainisha hayo kupitia ukurasa wake maalum wa facebook baada ya kupita siku moja tokea aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa (CUF) Jimbo la Mto Pepo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa (CUF) Wilaya ya Magharibi A. Zanzibar, Ali Juma Suleiman kufariki dunia katika hospitali ya Mnazi Mmoja kutokana na kile kinachoelezwa kuwa alivamiwa nyumbani kwake na kupigwa kisha baadaye kutupwa.
"Kuuawa kwa ndugu Ali Suleiman, Katibu wa Habari na Uenezi CUF, Wilaya ya Magharibi ni tukio lingine la kulaaniwa vikali. Kukalia kimya matukio ya namna Hii ni kukaribisha siasa ya damu kuzoeleka katika nchi yetu", amesema Zitto.
Pamoja na hayo Zitto ameendelea kwa kusema "Uchunguzi wa kina ufanyike kukomesha matukio ya namna hii, hakuna damu ya mtanzania inapaswa kumwagika kwa sababu ya siasa. Nawapa pole ndugu zetu wa CUF na wanazanzibar kwa msiba huu", amesisitiza Zitto.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni