Mishamo Tz

Jumamosi, 30 Septemba 2017

Quick Rocka Aipa tano Hallelujah ya Diamond"

Msanii wa muziki Bongo, Quick Rocka ametoa pongezi za kutosha kwa Diamond kufikisha kwa kufikisha views milioni moja ndani saa 15 katika mtndao wa YouTube.

Quick Rocka ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Still’ametumia ukurasa wake wa Instagram kutoa pongezi hizo na kueleza kuwa hatua hiyo ni recodi ambayo ni vigumu kuja kuvunjwa.

“Big shout out to Diamond, Hallelujah is dope tone, wewe mwenyewe umeua!, umeua!!, you know am say, so I appreciate good work bro, and the video is a movie , so big shout out to you,” amesema Quick.

“One million views in 15 hours that’s a record ujue hakuna mwingine atatokea avunje recodi hii ni ngumu sana kuvunjika, salute bro” amesisitiza.

Wimbo wa Diamond Hallelujah ulitoka September 28, 2017 ambao amewashirikisha Morgan Heritage hadi sasa katika mtandao wa YouTube una views 1,562,865.

Alikiba:Jiandaeni Kupokea kitu kipya"

Msanii Alikiba ameweka wazi mipango ya mkongwe wa muziki Abby Skillz, kuwa muda si mrefu atakuja na ngoma yake mpya baada ya ngoma yake ya 'Averina' ambayo alikuwa ameshirikishwa yeye pamoja na Mr Blue ambayo ilitoka mwaka jana.

Alikiba amesema hayo wakati akimpa pongezi mkongwe huyo baada ya kufanikiwa kufunga ndoa jana na mchumba wake Andoya khalifa Mrimi.

"Hongera mkongwe nakutakia kheri na mafanikio katika ndoa yako na ngoma mpya inafuata" aliandikwa Alikiba kupitia katika mtandao wake wa Instagram

Abby Skillz ni kati ya wasanii ambao walidaiwa kuwa chini ya usimamizi wa Alikiba kupitia 'Label' yake ya King's Music ambapo Alikiba aliwahi kusema kuwa baada ya kuachia wimbo wake mpya ambao ni 'Seduce Me' alisema baada ya hapo utakuwa ni wakati wa wasanii waliopo kwenye Label yake hiyo kutoka na ngoma zao pia.

PolePole Afunguka Haya"

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM), kimesema Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana hajahudhuria vikao vya kamati kuu na halmashauri kuu kwa kuwa aliomba udhuru wa kihali kwa kuwa anauguza ndugu yake wa karibu wa familia.

"Ndugu yetu Kinana anauguza ndugu yake wa karibu, tumwombee apone lakini Kinana alishiriki vyema kikao cha Sekretarieti. Kinana hajajiuzulu au kuandika barua ya kujiuzulu," amesema Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.

Chama hicho pia kimetangaza kuwachukulia hatua kali makada wake watakaobainika kukiuka utaratibu wa uchaguzi wa ndani wa chama hicho.

Polepole amesema hayo leo Jumamosi alipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za chama hicho Lumumba jijini hapa akitoa taarifa ya vikao vya juu vilivyoanza juzi Ikulu ya Dar es Salaam. Amesema Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amesema vikao hivyo vimepitisha majina ya wagombea wa uenyekiti ngazi ya wilaya.

Amesema kati ya wilaya 161 za kiserikali ambazo ni sawa na za kichama, kikao cha Kamati Kuu na Halmashauri Kuu iliyoketi leo Jumamosi  imezuia uchaguzi katika wilaya sita.

Amezitaja wilaya hizo kuwa Moshi Mjini, Siha, Hai na Makete kwa sababu waliojitokeza kugombea wameonekana kuwa watu hatarishi kwa chama hicho na uchaguzi utatangazwa baadaye.

Wilaya za Musoma Mjini na Musoma Vijijini zitarudia baada ya kutenganishwa kutoka wilaya moja na kuwa mbili.

"Chama hakitasita kuwachukulia hatua kali ikiwemo kufuta uchaguzi au kuwafukuza uanachama wale wote watakaobainika kutozingatia maadili na kanuni za chama chetu," amesema Polepole.

Amesema Halmashauri Kuu imetoa onyo kali kwa wanachama wa Zanzibar walioanza kampeni za uchaguzi mkuu ikisema muda bado na wakiendelea watachukuliwa hatua.

Mwananchi:

Diamond Afunguka Sababu ya Kuitosa Vevo

Dar es Salaam. Mwanamuziki Diamond Platnumz amelitolea ufafanuzi suala la mtandao wa YouTube na Vevo baada ya kuzuka sintofahamu kuhusiana na chaneli hizo mbili za kurushia nyimbo za wasanii.

Katika maelezo yake pia ametoa sababu za kuuita wimbo Hallelujah alioutoa juzi usiku. Wimbo huo uliowekwa saa 38 zilizopita umetazamwa na watu milioni1.6 katika mtandao wa YouTube.

Diamond amesema licha ya kujiunga na mtandao wa Vevo, aliamua kuachana nao kutokana na masuala ya maslahi kutomridhisha.

Amesema kulinganisha YouTube na Vevo kwa mtu anayejua masuala ya mitandao ni sawa na kulinganisha baba na mtoto.

“Vevo wanauza Youtube hivyo moja kwa moja mtandao ninaoutumia kuweka kazi zangu ndiyo ambao unanilipa zaidi na ndiyo mtandao mama, ni kweli niliingia Vevo hapo awali lakini kutokana na kushidwana kwenye maslahi niliamua kuachana nao,” amesema mwanamuziki huyo.

 Kwanini alitumia neno Hallelujah?

Meneja wa mwanamuziki huyo, Salaam Sharaf amesema jina la wimbo huo limetumika kama kionjo cha kusifu uumbaji wa Mungu na si kama wengi wanavyotafsiri.

Salaam hakuishia hapo alitolea mifano ya baadhi ya wasanii hapa nchini ambao wamewahi kuweka neno Mashaalah katika nyimbo zao, huku wengine wakitumia neno Halelluya maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi akiwemo mwanamuziki Nameless katika wimbo wake “Nasinzia”.

“Wakati anatunga mashairi yake lengo lilikuwa kusifia uumbaji, mbona wapo wasanii wengi hapa nchini wametumia neno Mashaallah, Hallelujah maana yake ni kumtukuza na kumsifu Mungu lina tofauti gani na Mashaalah?” amehoji Salaam.

Hata hivyo amesema watu wanaozungumzia suala hilo wanatafuta namna ya kuonekana wanaongea na iwapo wanaona kuna mahali mambo hayajakaa sawa ni vema wakaenda kwenye vyombo vya sheria, “Nafikiri hawana jipya wameshindwa watasema nini kuhusu wimbo huu, hawana sababu ya msingi.”

Waziri Ajiuzulu"

Waziri ajiuzulu
Mishamojr

Waziri wa afya nchini Marekani, Tom Price amejiuzulu baada ya kukodi ndege binasfi ikiwa ni kwa ajili ya shughuli za kiserikali.

Waziri Price aliomba radhi kwa kufanya safari akitumia ndege za kukodi mara 26 tangu mwezi May kwa gharama za dola za kimarekani 400,000 zikiwa ni fedha za walipa kodi nchini humo.

Nchini Marekani maafisa wa serikali isipokuwa wale wanaoshughulikia masuala ya usalama wanatakiwa kutumia ndege za abiria katika safari za kikazi. Habari zinasema mawaziri wengine watatu katika utawala wa Trump wanachunguzwa kwa kutumia ndege binafsi za kukodi kwa shughuli za serikali.

Taarifa ya Ikulu imesema Rais Trump ameridhia kujiuzulu kwa Price na tarifa hiyo kuainisha kwamba Don J Wright atakaimu nafasi hiyo kwa sasa Wright ni Naibu Waziri wa Afya katika serikali hiyo.

Mwigulu Aibua Upya Mjadala wa aliye mtolea Bastola

Kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kwamba mtu aliyemtolea bastola hadharani Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye si askari wa Jeshi la Polisi imeibua upya mjadala kuhusu suala hilo.

Waziri Mwigulu alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds baada ya mmoja wa wasikilizaji kutaka kujua kama mtu huyo aliyemtolea bastola Nape alikamatwa au hajakamatwa.

Baada ya kauli hiyo, wadadisi wa masuala ya kisiasa wametaka waziri Mwigulu ambaye Jeshi la Polisi liko chini yake kuueleza umma mtu huyo kama si askari ni nani au awachukulie hatua askari walioshindwa kumchukulia hatua mtu huyo.

Nape alikumbana na kadhia hiyo Machi 23 ikiwa ni saa chache kupita tangu Rais John Magufuli alipotangaza kumwondoa kwenye Baraza la Mawaziri akihudumu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Baada ya kuondolewa asubuhi, siku hiyohiyo mchana Nape alipanga kufanya mkutano na waandishi wa habari katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam ambako alikuta zuio la vyombo vya dola na alipolazimisha alijikuta akitolewa bastola mbele ya waandishi wa ndani na nje akitakiwa kurudi ndani ya gari lake na asifanye mkutano huo.

Tangu kutokea kwa tukio hilo, kumekuwapo mijadala hasa ikilenga kujua kwa nini hatua hazichukuliwi kwa mtu huyo licha ya video na picha mbalimbali zinazomwonyesha akitoa bastola na kumnyooshea Nape zipo na zinasambaa mitandaoni.

Mjadala huo ulitua katika Bunge la Bajeti lililokutana Aprili na hata katika mkutano wa Bunge uliomalizika wiki tatu zilizopita mjini Dodoma, baadhi ya wabunge wakitaka suala hilo na matukio mengine yajadiliwe ndani ya Bunge jambo ambalo halikufanyika.

Spika wa Bunge, Job Ndugai alichukua uamuzi wa kuitaka Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama chini ya Mwenyekiti wake, Balozi Adadi Rajabu kulishughulikia suala hilo na taarifa yake ilikuwa isomwe katika mkutano huo wa Bunge lakini ilishindikana na inatarajiwa kusomwa Novemba.

Juzi, waziri Mwigulu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi akijibu swali la msikilizaji kuhusu mtu huyo kukamatwa au la akisema: “Ninachofahamu aliyemtishia bastola Nape hakuwa polisi kama ambavyo ilidhaniwa.”

Alisema katika tukio kama hilo, wahalifu wanaweza kutumia nafasi hiyo kufanya watakavyo, lakini uchunguzi wa suala hilo unaendelea.

Jana, gazeti hili lilimtafuta Nape kutaka kujua maoni yake kuhusu kauli ya waziri Mwigulu ambaye alisema kwa kifupi: “Siwezi kuzungumzia hilo kwani sijaona… nikiona nitaweza kuzungumza.”

Itakumbukwa, Aprili 8 mwaka huu, Nape akizungumza jimboni kwake kwa mara ya kwanza tangu alipoondolewa katika nafasi ya uwaziri alisema hakuchaguliwa kwenda kuwa waziri bali kuwatumikia wananchi huku akitoa ushauri kwa Rais Magufuli.

“Namwomba Rais wangu, na huu ni ushauri tu, simlazimishi, ninampa ushauri na kumwomba… kwa sababu matendo haya yanamjengea chuki yeye na wananchi kwa sababu wanadhani yeye ndiye anaowatuma,” alisema.

Nape alisema, “Sasa ili Rais wangu asijengewe chuki lazima ajiondoe kwenye jambo hili na namna ya kujiondoa ni kuunda tume iende kuchunguza imletee ripoti nani yupo nyuma ya haya matendo ya kihuni.” Alisema, “Ili atenganishe CCM na matendo ya wahuni wachache wanaotumia dhamana waliyopewa kuumiza watu na kupoteza watu lazima tume iundwe iende ikatuletee ukweli, ngoja niseme hapa kwani si nipo nyumbani tu… kama nilitolewa bastola si ni sawa na kufa tu, basi nipo tayari.”

Atueleze ni nani

Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), John Seka akizungumza na gazeti hili kuhusu kauli ya waziri Mwigulu alisema inaashiria kwamba uchunguzi wa suala hilo la Nape umekamilika hivyo taarifa yake inapaswa kutolewa kwa wananchi.

“Kama waziri amesema si askari, anawajibu wa kusema ni nani, kwani ushahidi wa mazingira upo. Lakini kama hakuwa askari alikuwa ni nani, je, anaruhusiwa kumiliki silaha na je, alitumwa na nani kwa lengo gani,” alihoji Seka.

Alisema, “Na kauli hiyo ya waziri inaashiria uchunguzi umekamilika na kubaini kwamba si askari… nilitarajia jana (juzi) wangemuuliza pale kama si askari wa Jeshi la Polisi ni nani kwani kwa kauli hiyo uchunguzi unaonesha umekamilika.”

Alipoulizwa na gazeti hili kuhusu hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu alisema: “Siwezi kuyazungumzia masuala hayo katika simu, ‘next week’ nitakuwa bungeni Dodoma utanitafuta.”

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu, Ernest Mangu alisema, “Sina hiyo fursa, waulize walio kwenye nafasi hiyo.”

Alipoulizwa kwamba anaweza kutoa maoni yake na yakafanyiwa kazi ili huyo asiyejulikana akajulikana, Mangu alisema, “Kama watahitaji wataniuliza, wewe unaniuliza kama nani, hayo ni masuala ya kiutendaji.”

Polisi wawajibishwe

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRD), Onesmo ole Ngurumwa alisema kauli ya waziri Mwigulu inazua utata hasa ikizingatiwa Nape alizuiwa kufanya mkutano na aliyetoa bastola aliitoa mbele ya askari wakishuhudia.

“Kitendo cha yule kutoa silaha mbele ya askari tena na RPC Kaganda (aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda) alikuwepo na akaachwa inaonyesha wanamjua ni mwenzao, kama si mwenzao au hawamjui, ilikuwaje atoe silaha hadharani na wamwache bila kumchukulia hatua,” alihoji.

Ole Ngurumwa alisema, “Kama ndivyo, basi Mwigulu awachukulie hatua askari wake waliokuwepo wakati huyo asiyejulikana anatoa bastola kwani ni kosa kutoa silaha hadharani tena mbele ya askari.”

Kauli ya kwanza ya Mwigulu

Itakumbukwa Machi 24 ikiwa ni siku moja tangu Nape kunyooshewa bastola, waziri Mwigulu alitumia akaunti yake ya mtandao wa kijamii kuzungumzia sakata hilo akisema, “Mh. Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni Mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu.”

“Kitendo cha mtu kumtolea bastola, sio cha kiaskari, sio cha Kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa bastola mbele ya kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini,” alisema.

Alisema, “Nahusika na usalama wa raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP (Inspekta Jenerali wa Polisi) atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari, na kama ni askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake,” alisema

Ndo Ya Zamaradi yaleta Mjadara Mtandaoni"

Ndoa ya mtangazaji wa kipindi cha Take One kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds, Zamaradi Mketema imezua mijadala mtandaoni, huku wengi wakihoji iwapo ni kazi mpya ya sanaa ya mwandaaji huyo wa filamu ya Kigodoro.

Hata hivyo, taarifa zilizosambaa mtandaoni tangu usiku wa kuamkia leo Jumamosi zinaeleza mtangazaji huyo ameolewa na ndugu wa karibu wa kiongozi katika Serikali ya Awamu ya Tano.

Zamaradi kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka picha ya harusi yake, huku sura ya bwana harusi ikiwa haionekani vizuri na kuandika 'Alhamdulilah'.

Katika mitandao baadhi ya watu wamepongeza mtangazaji huyo huku wengine wakionyesha kushangazwa na tukio hilo kwa madai kuwa limekuwa ni la muda mfupi.

Rafiki wa karibu wa mwanadada huyo, Faiza Ally amempongeza kupitia ukurasa wake wa Istagram kwa kuandikia, “Ndoa yako iwe ya kheri Inshaallah.”

Mwingine aliyetuma ujumbe ni Jumalokole2 aliyeandika kupitia ukurasa wake wa Istagram akisema, “Wanawake wote mnapaswa kumuiga @zamaradimketema nimependa sana sema nyie mwalimu wenu......mwenzenu katumia fursa ..kaacha mbili kaifuata 6.”

Baadhi ya wasanii nchini wamempongeza kupitia mitandao ya kijamii. Msanii wa filamu Johari Chagula ameandika kwenye mtandao wa Instagram akisema, “Hongera sana Zama Mungu akuongeze vyema katika maisha mapya hakuna kitu kizuri kama amani ya nafsi furaha ya moyo, hakika hakuna kinachoshindikana chini ya jua, Nina hakika nitafuata nyuma.”

Zitto Kabwe Atoa Neno Juu ya Mauaji ya Polisi kufanya Uchunguzi

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe amelitaka Jeshi la Polisi kufanyia uchunguzi wa kina matukio ya kiuhalifu yanayopelekea kuuawa kwa viongozi kwa madai kitendo hicho kinakaribisha siasa ya damu kuzoeleka katika taifa

Zitto amebainisha hayo kupitia ukurasa wake maalum wa facebook baada ya kupita siku moja tokea aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa (CUF) Jimbo la Mto Pepo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa (CUF) Wilaya ya Magharibi A. Zanzibar, Ali Juma Suleiman kufariki dunia katika hospitali ya Mnazi Mmoja kutokana na kile kinachoelezwa kuwa alivamiwa nyumbani kwake na kupigwa kisha baadaye kutupwa.
"Kuuawa kwa ndugu Ali Suleiman, Katibu wa Habari na Uenezi CUF, Wilaya ya Magharibi ni tukio lingine la kulaaniwa vikali. Kukalia kimya matukio ya namna Hii ni kukaribisha siasa ya damu kuzoeleka katika nchi yetu", amesema Zitto.
Pamoja na hayo Zitto ameendelea kwa kusema "Uchunguzi wa kina ufanyike kukomesha matukio ya namna hii, hakuna damu ya mtanzania inapaswa kumwagika kwa sababu ya siasa. Nawapa pole ndugu zetu wa CUF na wanazanzibar kwa msiba huu", amesisitiza Zitto.

yanga ya jingamba kuichakaza mtibwa sugar

Yanga yajigamba kuichakaza mtibwa sugar

YANGA leo inacheza na Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, lakini imetamba kushinda.

Wakati Mtibwa ikiwa kileleni, Yanga yenyewe ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi nane, lakini kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa amesema kuwa wamejiandaa kushinda mchezo huo.
Nsajigwa alisema wanataka kushinda mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wao.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Nsajigwa alisema wanajua Mtibwa ni timu nzuri iliyojiandaa kwa ushindani msimu huu lakini watakabiliana nayo ili kuhakikisha wanapata ushindi.

“Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika mechi yetu na Mtibwa japokuwa naamini itakuwa na ushindani mkubwa kwani wapinzani wetu wapo vizuri msimu huu.
“Katika mechi hiyo tutamkosa Tshishimbi (Papy Kabamba ana kadi tatu za njano) lakini nafasi yake kuna mchezaji ambaye tayari tumemwandaa kwa ajili ya kuiziba hivyo ni matumaini yetu kuwa tutafanya vizuri,” alisema Nsajigwa.

Kwa upande wake, Kocha wa Mtibwa, Zuberi Katwila amesema moto walioanza nao msimu huu ndiyo huohuo watakaoendelea nao leo dhidi ya Yanga.

“Tunaiheshimu Yanga lakini kwa sasa sisi ni bora kuliko wao na ndiyo maana tunaongoza ligi kwa hiyo tumejipanga kuhakikisha tunaibuka na ushindi,” alisema Katwila.