Mishamo Tz

Jumapili, 14 Mei 2023

Gudluck Inocent Sostenes

​Gudluck Inocent sostenes magulu amezaliwa

29/08/2020

Katika Hospital ya Mwabui iliyopo mkoa wa mwanza Kata ya nyanguge wilaya ya magu

amezaliwa Saa 9:05 usiku siku ya jumamosi

Jumatano, 19 Oktoba 2022

WALI WA PILAU

​WALI WA PILAU

viambata


Mchele kilo 1


Nyama kilo 1


Samli  kilo


Vitunguu maji  kilo


Vitunguu thomu gram 100


Tangawizi mbichi gram 100


Mdalasini gram 50


Hiliki gram 25


Pilipili manga gram 100


Zabibu gram 100


Chumvi kiasi


1                    Teleka nyama utie chumvi na maji uipike mpaka iive. Baadae epua uiweke (ubakishe supu itakayotosha kuweza kuivisha mchele).


2                    Menya vitunguu uvikate. Menya vitunguu thomu na tangawizi mbichi utwange pamoja. Menya hiliki uitwange pamoja na bizari nzima. osha vijiti vya mdalasini pamoja na chembe za pilipilimanga uziweke. Osha zabibu uziweke. Menya mbatata uzioshe uziweke.


3                    Teleka sufuria tia samli, ikichemka tia vitunguu uvikaange. Tia thomu na tangawizi mbichi uliyoisaga tia vipande vyote vya nyama bila supu, tia mbatata na viungo vyote ulivyovisaga na kuviosha, isipokuwa zabibu. Kaanga kwa muda mfupi, baadae tia supu yote. Ikianza kuchemka tia mchele, onja chumvi. Angalia kiini cha mchele, ukiona wali umeiva na kukauka, fukua kati utie zabibu zote na baadae funika upalie moto.

Jumatano, 21 Septemba 2022

JINSI YA KUPIKA VIAZI VYA NYAMA VYA NAZI

​JINSI YA KUPIKA VIAZI VYA NYAMA VYA NAZI(STYLE 2)


 



Miongoni mwa vyakula vinavyonidondosha mate na kunifanya nile mpaka nivimbiwe ni viazi vya nazi. Ninapoulizwa nyumbani ni chakula gani tupike basi viazi vya nazi havikosekani kwenye orodha. Naam! Viazi vya nazi ni chakula maarufu mno Mombasa na kote pwani Kwa ujumla. Vile vile ni chakula ambacho kwamba ni nadra sana kukosekana wakati wa ramadhani.  Pengine huenda kisipikwe mwaka mzima lakini Ramadhani ni lazima kitapikwa japo siku chache. Hili ni dhihirisho kuwa ni chakula kinachoenziwa na wengi. Bila shaka kama hukifahamu chakula hiki basi una hamu kuu ya kujua kinavyoandiliwa. Ungana nami tujifunze Kwa pamoja! Kumbuka! Raha ya viazi vya nazi ni vikolee nazi.


MAHITAJI


viazi kilo 1 vilivyochambuliwa maganda na kukatwa Kwa slices (hakikisha slices si nyembamba sana ili viazi visivurugike)

Nyama 1/2 kilo iliochemshwa na Chumvi (usiiache na supu nyingi kwasababu kuna matusha)

Tomato 2

Kitunguu maji 1

Pilipili boga/hoho 1

Dania 1

Kitunguu thomu kilichosagwa kijiko 1 cha mezani

Curry powder kijiko 1 cha mezani

Matusha(tui jepesi) vikombe 3

Tui zito kikombe 1

Chumvi kiasi


MATAYARISHO


Weka viazi kwenye sufuria kisha ukatie Katia ndani yake tomato,  Kitunguu maji,pilipili  boga na dania

Weka Kitunguu thomu, currypowder, chumvi na matusha ufunike viazi vyako viendelee kuiva Kwa moto wa kiasi

Kama viazi bado vigumu utaongeza matusha kidogo(hakikisha umeweka matusha ya akiba pembeni)

Viazi vikielekea kuiva weka nyama(kama nyama ni ngumu Sana unaweza ukaiweka mwanzoni wakati ukiweka tomato na vengivyengi)

Viazi vikishaiva, weka tui zito(unaweza ukaweka royco  ukakorogea ukipenda)

Acha itokote Kwa dakika 3 na viazi vipo tayari

Andaa Kwa pilipili ya ndimu

Jumatatu, 29 Oktoba 2018

MAPISHI YA CHICKEN SATAY

Mapishi ya Chicken Satay

Chef 
Mishamo

Mahitaji

Kidali cha kuku 1 (chicken breast)

Kitunguu maji 1/2 (onion)

Kitunguu swaum/tangawizi (garlic and ginger

paste) 1 kijiko cha chai

Limao ( lemon)1/4 kijiko cha chai

Curry powder 1/4 kijiko cha chai

Pilipili ya unga kidogo (Chilli powder)

Coriander powder 1/4 kijiko cha chai

Soy sauce 1kijiko cha chai

Mafuta 2 vijiko vya chai.

Chumvi kiasi (salt)

Vijiti vya mishkaki

Matayarisho

Osha kidali kisha kikaushe maji na kitchen towel na ukate vipande(cubes) vidogodogo na uweke pembeni. Baada ya hapo changanya vitu vyote

(kasoro vijiti )na utie vimaji kidogo kisha visage katika breda kupata paste nzito. Baada ya hapo changanya hiyo paste na kuku na uache

zimarinate kwa muda wa saa moja. Baada ya hapo zitunge kuku katika vijiti vya kuchomea na uzichome katika oven mpaka ziive (inaweza kuchukua kama dakika 10). Baada ya hapo chicke

Jumamosi, 15 Septemba 2018

Kashata za maziwa ya unga

KASHATA ZA MAZIWA YA UNGA

MAHITAJI

Maziwa ya unga kikombe 1 na nusu

Sukari kikombe 1 na robo

Maji kikombe 1 na nusu

Arki ya vanilla kijiko 1 cha kula

Rangi ya chakula kjk 1 cha kul(orange)

Mafuta ya kupikia vjk 2 vya kula

MATAYARISHO

Kwenye sufuria au pan tia maji na sukari , wacha ichemke
Ikianza kutoa mapovu mazito ( dakika 8 hadi 10) tia rangi , arki na mafuta ya kupikia , koroga kg wacha ichemke tenaSubiria tena kwa dakika 3 mpaka 5 au iwe nzito ukiigusa kwa vidole viwili ukiwachia ifanye kama uzi au mfano wa gundi

Tia maziwa ya unga koroga haraka haraka kwa dkk 1 au mpaka mchanganyiko uwe mzito

Pakaza mafuta sehem yako ya kukatia au trey , weka mchanganyiko wako, tumia mwiko,kijiko au kifimbo kuwekea sawa,  wacha upoe na ukate shape unayopenda

Faida 10 za kunywa maziwa

Faida 10 za Kunywa Maziwa Usizozifahamu

Maziwa hufanya mambo mengi mazuri kwa ajili ya afya yako. Wataalamu wa afya na wauzaji wa maziwa wamekuwa wakieleza faida kadha wa kadha za kunywa maziwa. Je umewahi kujiuliza hasa ni faida gani hizo zitokanazo na unywaji wa maziwa?

Ni wakati wako sasa wa kujiuliza kwa kina juu ya faida zitokanazo na unywaji wa maziwa. Fuatana nami katika makala hii nikueleze faida 10 zitokanazo na unywaji wa maziwa.

1. Hujenga na kulainisha ngozi

Je unamfahamu Cleopatra? Cleopatra alikuwa ni malikia wa Misri anaesadikiwa kuwa mzuri sana. Inaaminikia uzuri wa Cleopatra ulitokana na tabia yake ya kuogea maziwa mara kwa mara.

Hivyo basi, ni wazi kuwa, vitamini na virutubisho vilivyoko katika maziwa ni muhimu kwa ajili ya ngozi bora. Ni vyema kunywa angalau bilauri moja ya maziwa kila siku.

2. Huimarisha meno

Maziwa ni chanzo bora cha madini ya kalisiamu, hivyo basi maziwa ndicho kitu halisi kinachohitajiwa na meno yetu. Pia maziwa huzuia kutoboka na kuoza kwa meno. Kalisiamu hufyonzwa na miili yetu kukiwa na vitamini D; hivyo jitahidi kunywa maziwa kwani maziwa huwa na vitamini D.

3. Huimarisha mifupa

Ni ukweli usiopingika kuwa watoto wanahitaji kunywa maziwa ili kuimarisha ukuaji wao. Ni kweli pia watu wazima wanahitaji kunywa maziwa ili kulinda na kuimarisha mifupa yao dhidi ya magonjwa kama vile udhaifu wa mifupa (osteoporosis). Maradhi haya huzuiliwa kwa kalisiamu ipatikanayo kwenye maziwa na ambayo hufyonzwa kutokana na uwepo wa vitamini D.

4. Kujenga misuli

Maziwa yana mchango mkubwa katika ukuaji wa misuli. Hili ni kutokana na protini zinazopatikana katika maziwa. Wanariadha wengi hunywa maziwa baada ya mazoezi, hii ni kwa ajili ya kuupa mwili virutubisho vya kutosha kwa ajili ya kujijenga tena. Maziwa huzuia maumivu ya misuli pamoja na kurudisha ute ulipotea kwenye misuli wakati wa kazi mbalimbali.

5. Kupunguza uzito

Utafiti unaonesha kuwa wanawake wanaokunywa maziwa hupunguza uzito zaidi kuliko wale wasiokunywa. Inashuriwa kunywa maziwa wakati wa chakula cha jioni au unapokula matunda. Pia maziwa yanaweza kutumiwa kama kileta hamu ya kula yaani appetizer.

6. Huondoa msongo wa mawazo

Hebu fikiri juu ya vitamini na virutubisho vilivyoko kwenye maziwa; hivi huweza kuondoa msongo. Baada ya kazi nyingi za siku, inashauriwa kunywa angalau bilauri (glass) moja ya maziwa ya uvuguvugu. Hili litakusaidia kukuondolea msongo katika misuli na neva zako za fahamu.

7. Huzuia maumivu wakati wa hedhi

Wanawake wengi wanakabiliwa na maumivu wakati wa hedhi. Maziwa yamedhibitishwa kuzuia na kupunguza maumivu haya kwa kiasi kikubwa.

8. Huongeza nguvu za mwili

Je unaishiwa nguvu mapema au kuchoka sana? Kama jibu ni ndiyo, unahitaji virutubisho vilivyoko kwenye maziwa. Hivi vitaupa mwili wako nguvu mpya na kukufanya kuwa mwenye nguvu na furaha siku nzima.

9. Huondoa kiungulia

Kiungulia huwasumbua sana watu wengi. Kiungulia husababishwa na asidi zipatikanazo tumboni. Hivyo maziwa (ambayo si mgando) hutengeneza utando maalumu tumboni ambao hupambana na asidi hizi.

Kwa hiyo nywaji wa maziwa (ambayo si mgando) utakusaidia kupambana na tatizo la kiungulia ndani ya muda mfupi.

10. Hupambana na maradhi mengine

Kwa miongo kadhaa tafiti zimebaini kuwa maziwa huzuia magongwa kadha wa kadha. Magonjwa hayo ni kama vile shinikizo la damu na kiharusi. Inaaminika pia maziwa hupunguza lehemu (cholesterol) mwilini na kuongeza uwezo wa macho kuona. Baadhi ya watafiti wameeleza kuwa unywaji wa maziwa huzuia ania fulani za saratani.

Hitimisho

Yaliyozungumziwa hapa ni faida 10 za kunywa maziwa. Naamini umebaini kuwa maziwa yana manufaa mengi sana kwa ajili ya afya yako zaidi ya haya yaliyotajwa. Ni jambo jema kujizoesha kula vitu vya asili, kwani ndivyo huhitajiwa zaidi na mwili wa mwanadamu. Jizoeze kunywa angalau bilauri moja ya maziwa kila siku kwa ajili ya afya ya mwili wako.

Je una maoni gani kuhusu makala hii? Je wewe huwa unakunywa maziwa? Tuandikie maoni yako hapo chini kisha washirikishe na wengine. Karibu

JUICE YA UBUYU

JE UNAJUA JINSI YA KUTENGENEZA JUISI YA UBUYU???soma hapa.........

© Mishamo TZ

Miaka hii yakaribuni ubuyu umekua tunda lenye jina kubwa sana kwenye jamii yetu ya kitanzania,unasifika kwa kua na virutubisho vingi hasa calcium na Iron

Ubuyu hufaa sana kwa Wajawazito,watoto na wazee,kwani makundi haya yanauhitaji mkubwa wa calcium na iron.
Namna nzuri na rahisi ya kufanya ubuyu sehem ya lishe  ni kwa kuutumia kutengeneza juisi
Juisi ya ubuyu imekua maarufu sana katika jamii yetu na inapendwa sana.Mimi mwenyewe ni mmoja wa wapenzi wakubwa wa juice ya ubuyu.Ingawa unaweza changanya ubuyu na matunda mengine,mimi napenda kunywa juice ya ubuyu pekeyake.Wakati mwingine naiwekea rangi na kuongezea vanila ili tu kuipa sura na harufu ya tofauti.
Watu wengi hawachemshi juisi ya ubuyu,Jambo ambalo ni hatarishi ki afya.Chemsha ubuyu ili kuuwa vijidudu viletavyo magonjwa,ubuyu hupita kwenye mikono ya wengi kabla haujakufikia wewe mtumiaji,na pia hujui ulitunzwa katika mazingira gani.Ni vyema kuchukua taadhari kwa kuchemsha.

© MAHITAJI

Ubuyu(wa unga au wa mbegu)
Maji
Sukari

© NJIA

1.Chambua ubuyu,ondo uchafu wowote uliopo kwenye ubuyu

2.Katika sufuria,weka ubuyu kisha ongeza maji.Katika kila kipimo cha ubuyu ongeza maji mara tatu yake
Ubuyu wa mbegu vikombe 6  weka maji vikombe 9
Ubuyu wa unga  vikombe 3 weka maji vikombe 12

3.Funika sufuria kisha bandika jikoni,chemsha adi vitokote,vipe  angalau dakika nne za kutokotea.
002

Kumbuka maji unayotumia kuchemsha ubuyu ni maji ya bomba na si salama,hivyo ni muhim kuyapa  muda mzuri wa kuchemka ili juice yako iwe salama.

4.Juisiinapoanza tu kutokota ongeza sukari kwa ladha uipendayo kisha acha zile dakika nne za kutokota ziishe.Zima jiko acha juisi ipoe.
Napenda kuweka sukari ichemkie kwenye juice kwani inafanya juice ishikane na kua nzito.Sukari ikichemshwa inakawaida ya kua nzito.Kumbuka kwamba ubuyu ni mwepesi sana na juice yake kawaida hujitenga inapotulia,ubuyu waenda chini na maji yanabaki juu.Ukichemsha sukari inasaidia kuondoa hali hiyo.

5.Chuja juisi,ongeza maji kama unaona ni nzito sana,na ongeza sukari endapo ile uliyoweka awali haitoshi.Juisi tayari kwa kunywa.

Maelezo ya ziada.

Kama unampa mtoto mdogo juice hii,basi acha itulie ili unga au chembechembe za ubuyu ziende chini,kisha chukua juisi nyepesi iliyobaki juu nsio umpe mtoto.Juice ya ubuyu nzuri sana kwa mtoto kwani ina calcium kwa wingi.